Msemaji wa DMX 'Domenick Nati' amesema rapper huyo na Swizz Beatz
wameanza kufanya kazi pamoja kwenye album mpya ya Dog Man X ila mpaka
sasa hatujajua lini cd hio inatoka. Swizz Beats na Dmx wameonekana
pamoja miezi michache iliyopita kwenye tamasha la Alicia Keys.
Fahamu kuwa rapper Dmx amekuwa akikabiliwa na matatizo ya kisheria
pamoja na kuishiwa. Hivi karibuni alimwambia mtangazaji moja huko
Marekani kuwa amebakiwa na dolla 50 tu kwenye account yake ya benki so
huu utakuwa mpango mzuri wa kumrudisha tena juu rapper huyu.
Post a Comment