Na
Mohammed Mhina, wa Jeshi la Polisi
Serikali
ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeshauriwa kuungana na Serikali ya
Zanzibar katika nia yake ya kununua meli kubwa kwa ajili ya mizigo na abiria
ili kutoa huduma bora ya usafiri kati ya Dar es Salaam, Zanzibar na Pemba na
kuepusha ajali za mara kwa mara.
Ushauri
huo umetolewa na Mkurugenzi wa Mipango na Sera wa Chama cha Wakulima Tanzania
Kanda ya Zanzibar Bw. Rashid Yusufu Mchenga, ambapo amesema kuwa, pamoja na nia
nzuri ya Serikali ya Mapinduzi ya kununua meli kama huku ikijibana kibajeti kwa
kiasi kikubwa.
Bw.
Mchenga amesema maafa yaliyotokea kwa siku za hivi karibuni kutokana na kuzama
kwa meli kubwa tatu za abiri za Mv. FATIHI, Mv. SPAICE SLANDER na MV
SKAGIT inatokana na Serikali yenyewe kutokuwa na meli ya uhakika.
Amesema
kuwa matokeo ya ajali hizo yamewagusa karibu Watanzania wote na hivyo ukimya ya
Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika suala la ununuzi wa meli kubwa ya
Serikali ya mizigo na abiria haileti picha nzuri kwa wananchi wake wanaotegemea
usafiri wa majini kwao pamoja na mali zao.
”Tumechoka
kuona ama kusikia Watanzania wanapoteza maisha na mali zao kwa uzembe unaoweza
kuepukika”. Alisema Bw. Mchenga.
Amesema
kuwa katika kifungu namba 14 cha katiba ya Muungano kinaelezea wazi kabisa juu
ya haki ya kuishi na hivyo ajali za mara kwa mara zinazokatiza maisha ya
Watanzania wenzetu, ni kinyume na sheria hiyo.
Bw.
Mchenga amesema kama ilivyo katika kuimarisha huduma ya usafiri wa treni za
abiria na mizogo kwa mikoa ya Tanzania bara, pia kuna haja Serikali kuona
uwezekano wa makusudi wa kuimarisha usafiri wa abiria na mizigo majini kwa
maana ya bahari, maziwa na mito.
Amesema
usafiri kwenye Maziwa kama Viktoria, Tanganyika, Nyasa na katika vivuko kwenye
mito mikubwa kama Kirombero, Wami, Kagera, Pangani na Ruvu unaweza kukumbwa na
tatizo kama vivuko na madara hayo hayataangaliwa kwa ukaribu.
Ametilia
mfano meli ya Mv. Liemba inayosafarisha abiiria na mizigo kwenye ziwa Tanganyika
wanaofanya safari kati ya Kigoma nchini Tanzania na Buurundi kwamba imepitwa na
wakati na kuna haja ya Serikali kuona umuhimu wa kutafuta meli nyingine ili
maisha ya wasafiri kwenye eneo hilo yawe ya uhakika.
“Mimi
naona kuna haja ya Serikali kujitathimini na kujipanga upya kwa kuangalia
vipaumbele na kuimarisha vikosi vyetu vya uokoaji ili kusaidia kazi za uokozi
zitokeapo ajali.” Alisema Bw. Mchenga.
Post a Comment