Mgombea wa Chama cha ADC Mhe. Amani Ismail Rashid akisaini fomu ya
Matekeo ya Uchaguzi Mdogo wa Jimbola Kiembesamaki Zanzibar baada ya
kutangazwa mshindi.
Mshindi wa Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar Mhe.
Mahmuod Thabit Kombo, akizungumza na Waandishi wa habari na kutowa
shukrani kwa wapinga kura wake na WanaCCM waliomuunga mkono katika
safari ya Kampeni na kuahidi kutimiza ahadi zote alizoahidi kwa Wananchi
wa Jimbola Kiembesamaki na kuondo kero zote na kuwaletea maendeleo
katika jimbo lao.
Mgombea wa Chama cha SAU Ramadhani Simai akizungumza na Waandishi wa
habari na kumpongeza Mgombea wa CCM Mhe. Mahmuod Thabit Kombo kwa
ushindi wake aliopata katika zoezi hilo la uchaguzi mdogo wa jimbo la
Kiembesamaki na kuyapokea matokea hayo kwa mikonomiwili.
Mgombea wa Chama cha TADEA Mhe. Ali Mohammed Ali ameridhika na matokea
hayo yaUchaguzi na ameridhika na kukiri hakuna Mamluki waliopita kupiga
kura katika vituo hivyo na kusema waliopiga kura ni Wananchi wa
Kiembesamaki tafauti na vyama vingine wanaolalamikia matokea hayo kuwa
sio ya haki. Uchaguzi ulikuwa ni wa Huru na Haki.
Na kusema chama chake kinajipanga Upya kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.
Kiongozi wa Chama cha Siasa Zanzibar Mhe. Mshenga akielezea hali ya
Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Kiembesamaki uliokuwa ni wa Huru na Haki,
hakuna mizengo iliofanyika katika Uchaguzi huo, Amesema amatembelea
vituo vyote na kuridhika na hali ya upigaji kura kwa Wananchi wa jimbo
hilo, Uchaguzi umekwenda kwa Amani bila ya vurugu hali hii ndiyo
Ustaarabu wa Zanzibar kuwa na utulivu na amani wakati chaguzi.
Viongozi wa Chama cha ADC, wakibadilishana mawazo baada ya kutangazwa
mshindi wa kiti cha Uwakilishi jimbo la Kiembesamaki wakijipongeza kwa
ushindi walioupata wa kura 84 kwa mara ya kwanza kushiriki uchaguzi kwa
Zanzibar na kujipa moyo watafanikiwa katika Chaguzin Kuu mwaka 2015.
kutokana na matokeo hayo yanatia moyo kwa Chama chao.
Post a Comment