By
Unknown
•
4:11 AM
•
LINAH
•
MSANII
nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah Sanga maarufu kama Linah,
anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa Kihindi anayejulikana kwa
jina moja la Nagar.
Estelinah
Sanga 'Linah'. Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana
huyo aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu
na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda
mrefu sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii
huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na
inaonekana hii mimba
ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi
wake,” kilisema chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa
wakiambatana pamoja katika sehemu mbalimbali za starehe.
Chanzo
hicho kilisema Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati zake za
kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa albamu ya
Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini
baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo,
alipiga simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani
kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya
watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema
anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema
kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe
si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi,
ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema
bila kufafanua zaidi.MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Estelinah
Sanga maarufu kama Linah, anadaiwa kupewa ujauzito na kijana mmoja wa
Kihindi anayejulikana kwa jina moja la Nagar.
Estelinah
Sanga 'Linah'. Chanzo cha uhakika kimeliambia gazeti hili kuwa msichana
huyo aliyeibukia kutoka kituo cha kukuza vipaji cha THT, amekuwa karibu
na Mhindi huyo anayedaiwa kuishi Mbezi jijini Dar es Salaam kwa muda
mrefu sasa na kwamba mimba hiyo imeonekana kumfurahisha sana msanii
huyo.
“Huyu Nagar ni mpenzi wake wa muda mrefu na inaonekana hii
mimba ameipenda sana. Kila siku anamsifu huyo mpenzi wake,” kilisema
chanzo hicho kilichodai kuwa wawili hao wamekuwa wakiambatana pamoja
katika sehemu mbalimbali za starehe.
Chanzo
hicho kilisema Linah alikutana na mdosi huyo katika harakati zake za
kimuziki na kwamba jamaa ameoza mno kwa binti huyo, mkali wa albamu ya
Atatamani.
Linah alipopigiwa simu mara ya kwanza hakupokea, lakini
baada ya kutumiwa ujumbe mfupi wa maneno na kuulizwa kuhusu suala hilo,
alipiga simu na kukanusha vikali tuhuma hizo.
“Nani
kakwambia kama nina mimba? Hakuna kitu kama hicho, hayo ni maneno ya
watu wanasambaza mtaani, mimi hata sijui wananitaka nini,” alisema.
Alipoulizwa kama hata yeye amewahi kusikia habari hizo, alisema
anazisikia na kusisitiza kuwa siyo za kweli. Lakini alipotakiwa kusema
kama anamfahamu Nagar, alimtaka mwandishi kuachana na habari hizo.
“Wewe
si umeuliza habari za mimba? Sasa hayo mengine yanatoka wapi,
ulichotaka kujua nimekujibu, hayo mambo mengine achana nayo,” alisema
bila kufafanua zaidi.
SIMILAR ARTICLES
Post a Comment