Guru Ramadhani. Mkurugenzi Bomba fm Zanzibar.
Mkurugenzi
mtendaji wa Radio bora hapa zanzibar
Bomba fm Radio GURU RAMADHAN aliwaambia wafanya kazi wake katika kikao
kilichofanyika mapema mwezi huu wa pili.Pamoja na Agenda nyingine ambazo nyeti
zilizojadiliwa pia mkuregenzi huyo alidhamiria kuibua na kuendeleza vipaji vya wanamuziki wa
Zanzibar ambao kwa namna moja ama nyengine vipaji hivyo vinaonekana kupotea
bure .Mkurugenza aliwataka waendesha vipindi vya burudani kulipatia mkazo hilo
na kulitekeleza kwa umakini mkubwa.
Pia
mkurugenzi amefanya mabadiliko ya vipindi kadhaa pamoja maboresho yake,
sikiliza BOMBA FM RADIO zanzibar ili
ujue kilichobadilika mwaka 2014.
Uptowntz
ilikutana na mtangazaji wa Breakfast Bomba MB The Swaga/Mb Doctor yeye alikua
na haya ya kusema.
MB DOCTOR & PASHA.
MB. Doctor.
Wanamuziki wa Zanzibar wanatakiwa kuboresha nidham zao ili kufikia mafanikio,
pia aliwataka kuacha dharau kwa maana hakuna career ambayo inaweza kusonga
mbele bila nidham ndani yake. Pia aliwataka wasanii kufanya kazi zenye ubora na
kiwango cha juu ili kua na ushindani zaid katika soko la mziki Tanzania.
JABIR.Super
Jay International.Host wa show za kiburu FRIDAY & SAT,DAY NIGHT GROOVE.Alitirirka
ifuatavyo.
JABIR SUPER JAY
Mafanikio
hayapatikani mara moja kama baadhi ya wasanii wanavyodhani hapa Zanzibar.
Inatakiwa kila msanii anaejijua kua anakipaji ambacho kinahitaji kuendelezwa
kama Radio hii ilivyodhamiria kufanya hvyo bac kuchukua jitihada binafsi
kulinda na kutunza kipaji chake ili kupata mafanikio siku za usoni. Super Jay
pia alisisitiza Nidham kwa wasanii. Pamoja na hayo yote alisema kuhusu fursa
hii ambayo wasanii wa Zanzibar wanatakiwa kuitumia bila kuipoteza kwani huu ni
moyo wa uzalendo ambao umeoneshwa na mkurugenzi wa Bomba fm Zanzibar.
Pia
muandishi wa Blog hii alikutana na msanii wa mziki wa kizazi kipya toka maeneo
ya fuoni Dogo fani alipoomuuliza kuhusiana nidham mbovu za wasanii yeye pamoja
na wenzake dogo fani ilikiri kua kweli kuna baadhi ya wasanii wanadharau na
akasema kua wasipobadilika na kujitunza watashindwa kuzitumia fursa kama hizi
ambazo zinatolewa na Bomba fm. Ameenda mbali zaidi na kumpongeza mkurugenzi wa
Bomba fm katika jitihada zake za kuboresha mziki huu.
KAZI KWENU WASANII KUFANYA KAZI NZURI NA BORA ILI FURSA HII ISIPOTEE BURE.
Post a Comment