PICHA - MATUKIO YA ZANZIBAR MUSIC AWARDS 2015

Mkurugenzi wa Biashara Zanzibar Nd. Mohamed Baucha wa kulia akimkabidhi Tunzo ya Video bora ya mwaka muziki wa kizazi kipya Nassir Hassan (Vanila) mara baada ya kuibuka mshindi, tunzo hizo zimeandaliwa na Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar.


Mwanamitindo marufu wa Zanzibar Farouk Abdillahi akimkabidhi Tunzo ya Video bora mwaka ya Taraab Bi. Saada Nassor.
Meneja wa Zenji Entertainment Seif Moh'd (kushoto) akimkabidhi tunzo Mwanamuziki Bora wa kiume wa tarabu asili Cholo Ganun.
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Dkt. Mwinyihaji Makame akimkabidhi tunzo ya muandaaji bora wa Tamasha Zanzibar Music Award mwaka 2015 Mbunge wa Jimbo la Uzini na Mkurugenzi wa Redio ya Zenji FM Mohamed Seif Khatib katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Salama Hall Bwawani Mjini Zanzibar. 
Mgeni Rasmi Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora) Dkt. Mwinyihaji Makame katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa Kampuni ya Zanzibar Media Corporation LTD.
ANGALIA PICHA ZAIDI HAPA 

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates