Rapper Kanye West ni miongoni wa wasanii wa kubwa wa karne ya 21, pia ni mume wa mmoja wa mastaa wakubwa sana duniani Kim Kadarshian… camera
na waandishi wa habari humfuata kila sehemu kunasa matukio yake ya kila
siku, blogs na websites zinamuandika karibia kila siku pia… lakini
ukiacha haya yote naamini bado kuna vitu ambavyo huvijui kuhusu Kanye mtu wangu.
Baada ya kuacha shule Kanye West aliwahi kufanya kazi kwenye kampuni ya bima kama kijana wa ‘customer care’ lakini baada ya hapo Kanye alifanya nini?… haya ni mambo mengine 10 usiyoyajua kuhusu rapper Kanye West.
10. Kanye West anazungumza kichina na aliwahi kuishi China na mama yake kwa mwaka mmoja na kusoma darasa la tano huko.
09. Mama yake alikuwa analipa dola 2 ili kumshawishi Kanye West acheze muziki.
08. Alitengeneza beat yake ya kwanza kabisa akiwa darasa ya saba.
07. Alivyokuwa na miaka 13 Kanye West alikuwa analia sana baba yake akimkataza kunyoa kiduku.
06. Jina lake la kwanza la utani lilikua ‘Deep House’ na lilitokana na yeye kupenda kuvaa nguo za oversize kipindi hicho.
05. Baada ya kuacha shule Kanye West alifanya kazi kwenye kampuni ya bima kama customer care ili aweze kupata hela ya kulipa kodi yake ya nyumba ambayo ilikuwa ni chumba alichopanga kwenye nyumba ya mama yake.
04. Kabla ya kufanikiwa kimuziki, Kanye West alijaribu kufanya biashara ya kuuza nyumba (real estate) lakini akaona anapata hela ndogo sana.
03. Kwenye maisha yake alishawahi kufikiria kucheza picha za utupu mara mbili ili apate hela ya kutengeneza beats za muziki.
02. Kanye West aliuza beat yake ya kwanza kwa dola 8,800 ambayo kwa pesa ya Kitanzania ya sasa ni sawa na milion 20,240,000.
01. Mara nyingi Kanye West akiwa kwenye mikutano na mikutano hiyo isipoenda vizuri, rapper huyo hulia!
Post a Comment