Mara nyingi wasanii hupata fursa ya kusikiliza nyimbo za
wenzao zinapokuwa kwenye hatua ya kutayarishwa.
Ben Pol aliusikia wimbo wa Ommy Dimpoz kabla hata ya
kutoka na kumwambia kuwa utakuja kuwa tishio.
‘Unakumbuka niliwahi kukuambia kuhusu 'Baadae ,ona bro
,sasa nchi yote inaimba 'Baaadaeee eeeh'...hongeraaaa!!!,” ametweet Ben Pol
kumwambia Ommy Dimpoz.
“Nakumbuka broo thanxxx,” alijibu Ommy.
Baadaye ni wimbo wa pili wa Ommy Dimpoz kufanya vizuri
baada ya kuhit pia na wimbo wake wa kwanza, Nai Nai aliofanya na Ali Kiba.
Katika hatua nyingine Ben Pol amekuwa msanii wa kwanza
Tanzania kuzungumzia habari ya msanii maarufu wa Marekani Frank Ocean
kujitangaza kuwa ni shoga.
“Frank ocean anatuweka watu kwenye wakati mgumu ,ametoa
album kali huku amejitangaza kuwa yeye ni gay ,kumuacha kumsikiliza nayo ni
ishu,da!” amesema.
Hata hivyo hitmaker huyo wa ‘Nikikupata’ na mshindi wa
tuzo za Kili, anaamini kuwa scandal hiyo haimpunguzii uwezo wake katika muziki.
“Haishushi ,ila bado wabongo sisi hatuwaelewi mashoga
(mimi mbongo pia) ,ameni-dissapoint kidizain flani ,ila he's a gud singr/writer.”
Album ya Frank Ocean, Channel Orange ilikamata nafasi ya
pili kwenye chart ya Billboard 200 na nafasi ya kwanza kwenye Billboard
R&B/Hip-Hop Albums chart, kwa kuuza kopi 131,000 katika wiki ya kwanza.
Post a Comment