Justin Bieber anataka David Beckham awe kocha wa timu yake



Justin Bieber anataka kuanzisha timu ya soka huko Los Angeles na anataka mchezaji wa kulipwa wa Uingereza David Beckham awe kocha wa timu hiyo.
Bieber mwenye miaka 18- anataka kufuata nyayo za Robbie Williams na Vinnie Jones kwa kuanzisha timu za soka.
Timu ya Robbie inaitwa LA Vale na wakati Vinnie ana timu mbili,Hollywood United na Hollywood Allstars.
Justin alisema: "Nimekuwa nikicheza soka sana katika miaka miwili ama mitatu mpaka sasa. Nimekuwa nikifurahia sana.
Aliendelea kuliambia gazeti la Daily: "Mtu mmoja tu ambaye tunataka awe kocha wa timu, naye ni David Beckham.


David Beckham
"Sio kwamba tutakuwa tukicheza mechi kila wiki. Kiukweli tutakuwa tukicheza game tatu ama nne kwenye msimu.”
"Ntamuomba David mimi mwenyewe naamini atakubali.
Justin aliongeza kuwa mpenzi wake Selena Gomez na mke wa David, Victoria Beckham nao pia wanaweza kuhusishwa kwenye project hiyo.
"Nitawaomba  Selena na Victoria kama watapenda kuwa  cheerleaders wetu! 
But hey, that might be pushing it,” alisema.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates