Muuaji aliyeua watu 12 kwenye uzinduzi wa movie ya Batman alitumia madawa yaliyomuua star wa Batman, Heath Ledger


James Holmes muuaji wa watu 12

Mpaka mwaka mmoja uliopita James Eagan Holmes alionekana mwananchi wa kawaida tu wa Marekani. Kijana mzuri kabisa.
Mpenda michezo, mtu wa familia, msomi, kijana kutoka jiji la San Diego, California, alionekana kuwa na mambo makubwa mbele.
‘Alikuwa akiosha gari la wazazi wake, alicheza soka’ alisema Tom Mai, ambaye ni jirani wa familia ya Holmes kwa miaka 15.
 ‘Tulikuwa tukinywa pamoja wakati wa Christmas na aliwapa ‘cookies’ wanangu, alikuwa kijana wa kawaida wa kimarekani. Hakukuwa na kitu kibaya kwake.’ 

Alipona chupuchupu: Marcus Weaver akonesha majeraha ya risasi mkononi
Vilio
Eneo la tukio
Silaha aliyotumia
Juzi, Holmes, 24, akiwa na silaha nzito ikiwemo Remington shotgun, gobole aina ya AR-15 na zingine, aliamua kuyakatisha maisha ya wapenzi 12 wa filamu waliokuwa wameenda kutazama tolea jipya la filamu ya Batman huko Denver, Colorado.
Akiwa amedhamiria kumaliza kila aliyekuwa mbele yake na bila huruma hata chembe, Holmes aliwaua watu 12 akiwemo mtoto mdogo mwenye miaka sita, Veronica Moser. 

Jessica Ghawi miongoni mwa waliouawa
Pia aliwapa majeraha ya kudumu watu wengine 59, akiwemo mtoto mchanga mwenye miezi mitatu.
Baada ya kukamatwa mtu huyo alisema yeye ni Joker! Adui mkubwa wa  Batman, hakuna kingine! Akili yake ilikuwa inamtuma kuwa hapo alikuwa ndani ya movie hiyo. Punguani,bila shaka!
Juzi tena yakaibuka mengine kuhusu muuaji huyu kwamba mapema mwezi huu alikuwa amejiandikisha kwenye mtandao wa kutafuta wachumba wa AdultFriendFinder na akaandika kuwauliza wanajamvi “Mtanitembelea jela? (‘Will you visit me in prison?’) 


Kuna ripoti kuwa mama yake Arlene na baba yake Robert, meneja wa kampuni ya software anayeishi kwenye nyumba ya vyumba vinne  alijua tu bila hata kuuliza kuwa mtoto wake ndiye aliyehusika baada ya kusikia maujia hayo ya juzi Ijumaa.

Wazazi wake walikuwa wanajua kinachoendelea kwa mtoto wao huyo tangu mwaka jana. Alikuwa akipendelea kutembelea mitandao ya  ngono, akitumia madawa na kuwaacha majirani wa mjini mdogo wa Aurora uliopo jijini Denver na ishara kuwa kijana huyu alikuwa na matatizo makubwa.

Polisi wanaamini kuwa kijana huyo alikuwa amekuwa mlevi wa filamu za Batman na kuna ripoti ambazo bado hazijathibitishwa kuwa alijikuta akitumia sana dawa za kupunguza maumivu za Vicodin, ambazo zilikutwa kwenye mfumo wa damu wa muigizaji marehemu Heath Ledger, ambaye aliigiza kama Joker kwenye filamu ya Batman. Ledger alifariki kutokana na overdose mwaka 2008.
Mashuhuda

Hadharani, angalau wazazi wa Holmes hawasemi iwapo wanafahamu ama kukisia nini kilimfanya mtoto wao achukue uamuzi huo.

Watalaam, wanaamini kuwa Holmes alikuwa na tatizo la kisaikolojia ambalo lingekuja kulipuka katikati ya miaka 15 na 25.

Holmes alianza kusoma PhD ya neuroscience kwenye chuo kikuu cha dawa cha Colorado mjini Denver mwaka jana lakini aliacha mwezi uliopita.

Kozi ya mwisho aliyoichukua ilikuwa ni ya magonjwa ya akili na psychiatric disorders.

Awali alisoma kwenye chuo kikuu cha California ambako alipata first-class kwenye degree ya neuroscience.

Mkuu wa chuo hicho, Timothy White alisema Holmes alikuwa mwanafunzi mwenye akili.
Rais Obama akiwakumbuka marehemu siku ya ijumaa
Licha ya kuwa na shahada Holmes alilazimika kutafuta kazi kwenye mgahawa wa McDonald wa eneo analoishi baada ya kuhitimu mwaka 2010.
Mr Mai alisema: ‘Hakupata kazi hivyo aliamua kurudi shule kusomea udaktari wa falsafa.
Juzi usiku mama yake Holmes aliungana na mama yake nyumbani kwao San Diego ambako kulikuwa kumefurika waandishi wa habari. Baba yake aliwasili Colorado na kupelekwa jela aliyowekwa mwanae ambaye alikuwa amewekwa peke yake kwa usalama wake mwenyewe.
July 5 mwaka huu, Holmes alifundua akaunti kwenye mtandao huo wa kutafuta wachumba kwa jina la ‘ClassicJimbo’. 

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates