Mama yake na Michael Jackson apotea, hajulikani alipo




Mtandao wa TMZ umeripoti kuwa mama yake na hayati Michael Jackson, Katherine hajulikani alipo.

Mtoto wa Michael Paris Jackson amethibitisha taarifa hizo kwa kutweet, "yes, my grandmother is missing. I haven't spoken with her in a week I want her home now."

 Aliendelea kuandika na kuwaomba watu ama mamlaka zifuatilie: "the same doctor that testified on behalf of dr murray saying my father was a drug addict (a lie) is caring for my grandmother... just saying."

Mwanasheria wa Katherine Jackson ameiambia CNN kuwa hajaonekana ndani ya saa 24 sasa wala kuwasiliana na wajukuu zake.

Kuna taarifa ya kuwepo kwa ugomvi mkubwa kwenye familia hiyo uliosababishwa na malumbano juu ya nyumba ya Michael kiasi cha kumfanya mama yake apatwe kiharusi cha kati.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates