Video: Mdogo wake Barack Obama bado choka mbaya


Mdogo wake na rais wa Barack Obama wa Marekani, George Obama bado ameendelea kuishi maisha magumu kwenye nyumba ya matope (slum) nchini Kenya.
“Nadhani ana familia yake mwenyewe,” alisema George Obama katika mahojiano na mwandishi Dinesh D’Souza.
“Mimi ni member wa familia yake lakini nina umri mkubwa, hivyo najisaidia mwenyewe,” mdogo wake na Obama alisema kwenye clip hiyo ya dakika nne iliyopo kwenye website ya Hollywood Reporter (www.hollywoodreporter.com).
D’Souza, mwandishi wa kitabu cha mwaka 2011 kilichouza sana “The Roots of Obama’s Rage,” alisema alimtafuta mdogo wake na Obama baada kumuona kwenye habari iliyomwonesha akiishi kwenye kijibanda jijini Nairobi.
Alipoulizwa na mwandishi huyo iwapo kaka yake ameshindwa kumsaidia George Obama alijibu: “Ana mambo mengine ya kushughulikia.”

“He’s taking care of the world, so he’s taking care of me.”

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates