Maelfu wampokea Marehemu Ngwea











Mwili wa aliyekuwa msanii mahiri katika game ya Bongo Flava hapa Tanzania, Albert Mangwea umewasili leo nchini kutokea Afrika Kusini na kupokelewa na umati wa ndugu, marafiki na mashabiki wa kazi zake ambao kila mmoja ameguswa kwa namna yake na msiba huu mkubwa, Na hii ni tayari kwa shughuli za kutoa heshima za mwisho hapa jijini Dar siku ya kesho kabla ya kuelekea Morogoro kwaajili ya maziko.

Hali imekuwa ni ya hamaki na huzuni katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere wakati wa kuwasili kwa mwili huu ambapo hii ndiyo hali halisi ilivyokuwa.

Wasanii mbalimbali wameweza kujitokeza ikiwepo kubeba msalaba na kusindikiza gari lililokuwa limebeba mwili wa marehemu na sehemu kubwa ya watu wakiwa wanataka jeneza lishushe kwenye gari na kubebwa na wao.

Raia hawa waliojitokeza kwa maelfu walikuwa wakiimba nyimbo mbalimbali za kuonyesha ni kwa jinsi
gani walikuwa wakimpenda marehemu

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates