ALL IN ALL SEHEMU YA KWANZA 1




SEHEMU YA KWANZA
   Jua kali la saa 9 lilikuwa linawaka kupita maelezo, Rashid ni kijana mwenye uchu wa maendeleo alipenda kujituma kama mtumwa akiwa na lengo la kuishi kama mfalme, wakati huu Rashid alikuwa kibaruani maeneo ya Raha leo pale linapojengwa ghorofa, hapa palikuwa na mchanganyiko wa wanaume na wanawake watoto na watu wazima palikuwa na wakandarasi kutoka India na Tanzania Bara, kila mtu alikuwa akisghulika  kufanya kazi aliyopangiwa lakini bado kulikuwa na unyanyasaji kutoka kwa wasimamizi wao.    
“Wewe mpumbavu tena mzembe kabisa masaa mawili unachanganya mchanga uwo kama umeshindwa kazi ni bora useme mjinga wewe kuna watu kibao ambao wanatafuta kazi wewe umepata unaizembea nasema kama huwezi kazi nenda kapakatane na mzee walo nyumbani..”  Rashid alitolewa maneno makali yaliochangayika na matusi ya nguoni.
Lakini bosi……. Rashid alijaribu kujitetea lakini hafla alikatishwa na bos wake “lakini kitu gani tena hakuna malipo leo mana sjaona la mana ulofanya tangu asubuhi.” Yule msimamizi aliyekuwa akisimamia kundi la akina Rashid aliondoka huku akionesha ni mwenye hasira na kumuacha Rashid akiwa ameduwaa.
……..
  Ilivyofika saa kumi na mbili za jioni ulikuwa mda wa malipo kwa wafanya kazi walikuwa wamejinga mstari mmjoa ulio kuwa mrefu.
“Ipo kuja haraka nasubiri nini hapa …” Muhindi alikuwa akimuhimiza moja wa kibarua ambae imefika zamu yake kwenda juchukua malipo, aliangalia jina lake na kusema ok nimeona jina yako nalipa elfu nne ….. waliendelea kwa mfumo uleule hadi zamu ya Rashid imefika  sema haraka naitwa nani? Muhindi alimuharakiza Rashid ambae alionekana kama amechoka kutokana na kazi aliofanya “Rashid ..Rashid naitwa ….” Rashid alijibu haraka haraka na Yule Muhind alikuwa akiangalia kwa makini lakini hakuliona jina la Rashid “wewe mbona natania mimi hapana ona jina la Rashid mimi ipo nafanya mchezo sio pisha nyengne apaa”… Rashid aliduwa na kutojua nini cha kufanya, ilimlazimu aandoke maeneo ya pale na kuelekea Daraja bovu kwani ndipo alipokuwa anakaa.
Wakati huu ilikuwa magharibi imeshaingia akapita njia ya Kwahaji tumbo na kuitafuta Makadara huku akiwa amechoka,Rashid alikuwa mrefu kiasi na sio mpana sana pia mweusi kiasi kwa upande wa ngozi yake ya mwili hapa alikuwa amevaa pensi ya kak iliyochafuka kwa saruji pia alikua juu alikuwa amevaa shart nyeusi pia inaonekana kama imechakaa, wakiti alipokuwa njiani hakuwa akikazana kwani alionekana kama amechoka pia mwenye mawazo baadhi ya mda alikuwa kama akiongeqa peke yako na kujishtukia wakati anapo pishana na watu.
Kitu kilichokuwa kimfariji njiani na kusahau yale yalotekea pale Rahaleo na kumpa nguvu ya kutembea ni Radio ambazo alikuwa anaziskia njiani haswa ambazo zilikuwa na program za music   alikua akizifuatishia kila nyimbo anayosikia alikua akipata hasira kila anaposikia nyimbo iliyokuwa haina  kiwango kizuri kwani yeye kuhangaika kote huko kulikua ni kutafatuta pesa ya kwenda studio  na wakati mwengine alikua akihisi kama anafanyiwa interview kwenye radio  kumbe anajiuliza maswali mwenyewe na kujijibu.
………………………..
Shikamoo mama.. Rashid alimsalimia mama yake aliyekuwa amekaa barazani. “Marhaba! Za uko utokapo?”   Bi Key mama yake na Rashid alimuitikia salamu, “Salama tu mama vipi chakula tayari mana nina njaa hatari mama kazi leo ilikuwa ngumu.” Rashid alilalama kwa mama yake. Mwanangu riski imepatikana hivi jioni nimeuza ule mkoba wa ukili tena pesa nimepewa nusu nasubir maji yapate moto nikabandike ugali subiri kidogo.” Bi key alimjibu Rashidi lakini Rashid hakuonesha kufurahia na majibu aliyopewa kutoka na njaa iliyokuwaikimparama alihisi kama tumboni kuna simba anamparura na makucha yake, aliingia ndani akiwa na mawazo ya kuenda kuoga. “Aghaaa shit”, Rashid alisema huku akizipiga mateke ndoo za maji mana zilionekana zikiwa tupu ikabidi achukuwe na kwenda mferejini kuenda kutafuta maji,
   Wakati alipofika mferejini alikuta umati w watu wakisubiri maji ikamlazimu akae foleni, mara alitokea Yahya rafiki yakme na Rashidi ambae alionekana akiwa mardadi alivaa shati ya rangi nyeupe na suruali aina ya jeans rangi nyeupe pia chini alivaa raba aina ya All star na mkononi alikuwa na saa aina ya Lacoste. Vipi Chidi!  Yahya alimsalimia rafiki yake Rashid ambae mara nyingi alipenda kumuita kwa kumkatisha jina na kumita Chidi. "poa inakuaje chif?" Rashid alimuitikia salamu Yahya na kumbambika suala "vipi naona umetokelezea wapi tena? Yahya alitabasamu na kumjibu Rashidi "ahh wapi kawaida tu naenda kwa shemegi yako Latifa si unajua tena...." Dah nakukubali kaka vipi Najma kwani au ndo ushapotea? Rashid alimuliza suala Yahya huku akionesha tabasamu na kujawa hamu ya kutaka kujua. Yahya alimjibu kwa mbwembwe nyingi Rashid "wewe vipi Najma ndo mwanamke wa malengo yangu hawa wengine nazingua tu kutoa baridi mwilini"  Rashid alicheka kwa kicheko kisicho na kawaida hadi watu wote pale mferejini wakawa wana jiuliza kulikoni, mara simu ya Yahya iliita   "Oyo sasa me nasepa namuwahi huyu mana do ananiharakiza kama vipi nitgakutafuta mana nimesikia tangazo redio kuwa wanatafuta vipaji vipi umesikiaa" Rashid alionekana kuduwaa  "hapana sijasikiaa....."
USIKOSE KUFATILIA SEHEMU YA PILI       

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates