MUZIKI WETU UNA MATUKIO MENGI SANA SANA!!! by Roma mkatoliki

Kama miaka 2 iliyopita hivi kulikuwa na show ya X -MASS MWANZA!! aaaf kesho yake 26th ilikuwa MUSOMA!! ilikuwa ni mimi na belle 9 na band fulani hii ya wakongo!!!

Sasa kiufupi tu ile show ya 25th ya X -MASS pale GOLD CREST MWANZA ilifeli hivi(obvious haikutangazwa so wakaifelisha
wenyewe waandazi)!!
lakini sisi mtonyo wetu tulikuwa tumeshabeba bfr!!

So kutokana na hali ile yule big boss akatutengenezea picha fulani hivi asubuhi ya kesho yake tulipoamka tu!!

Yeye alitaka tukafanye show ya bure musoma kesho yake kama kulipizia show yake ya mwanza iliyofeli.....
TULIPOKATAA jamaa akatumia UTARIME WAKE/ UBABE NA KUJUANA NA WADAU WA MWANZA AKATUITIA POLICE ASUBUHI PALE HOTELINI...anajua mwenyewe alivyowapiga kiswahili askari hadi wakajaa!!

Wana tukabebwa nini..... haoooooo hadi kituoni!!!
Sasa kwakuwa jana yake ilikuwa sikukuu, basi walikuwa wamekamatwa vijana wengi sana kwa makosa mbali mbali wakiwa mahabusu ya pale......

Aisee vile tunafika tu tunaambiwa aya vua mikanda/viatu/ aaaf ingieni kule kwa wenzenu!!!
sasa mle ndani nikipatazama na mwanangu belle 9 naona zile mbavu mule...duuuh!!! moyoni sasa nawaza itakuwaje kule ndichi!!

Aaaf sasa kiukweli mm sikuwa na wasi wasi kuhusu mimi, kiukweli!! coz najua kule wanangu wanaonielewa na muziki wangu watakuwa wengi tu lazima!!

Sasa wasi wasi nikawa ninao kwa bele 9(watamuelewa??!!)!! aaf tukiwa tupo pale kaunta tunaandikisha maelezo kule ndani wana wakaanza kuongea

"aisee rire si riroma riree..."
mwingine anajibu
"ee riko na ribere naini asee itakuwa wameshazingua"

wakaedelea kusema kwa sauti
" wana msijari karibuni humu ni kwa kira mtu juzi tu turikuwa naa ritwente pasenti na daz baba, huku ni kwa wote"

Daahh apo tunaandikisha maelezo tuna hasira na police wote wamekaza kama hawatujui...na yule boss sijui aliwapanga vipi hadi jamaa wakatukazia vile!!
basi kuna police flani wa kike mjeuri huyo akamtazama belle 9 kwa dharau aaf akauliza wee jina lako nani? anamuuliza belle kwa sauti...

basi nikasikia voko moja imetoka mle ndani mahabusu....

"issshhh ritazame rire ridemu ris....(tusi) eti anauriza belle 9 ni nani, akati simu yake rimejaza majimbo yake, yani we dada ni mus.....(tusi)"

duuuh tukamalize wana tukawa tunaingia ndani!! basi kufika tu tunaingia kuna mwana nakumbuka akamdaka belle fasta na kumkazia eti amvulie culture fulani hivi belle alivaa mkononi!
belle akamkazia aaf wakaanza kupandishiana pale pale huyu akitukana belle kajibu nayeye...daaah nikasema yeeees mtoto wa moro ninja kweli!!

Basi kuna wana mle ndani wakaanza zile za "oya kausheni kausheni hawa wana mjue, haya ndiyo majembe, oyaa mkatoriki eeee tulia apo chini msijali apa amani tu!!(hao wana wawili waliokuwa na sauti mle ndani ya kuweza kuwatuliza woote aisee sisahau sura zao hadi leo, maana walituelewa sana!!)
basi tukatulia...

Huku nyuma sasa report zimewafikia wana, maana jana yake sikukuu so mwanza kulikuwa na show kama nne hivi sehemu tofauti!!
alikuwa izzo b, linna,tunda, tip top wote... basi fasta pale kituoni akaja madee/barnaba na wana kibao kuja kujua kinachoendelea....


Sasa mle ndani aisee kwa haraka haraka tulikuwa sio chini ya 20 aisee na zaidi nahisi, yani tumebanana sana!!
asa kuna muda nimekaa nimesizi nawaza tuuu tunafanyaje hapa...
basi nasikia wana wanaambiana

"apo riroma rinatunga sheria apo rikitoka nheeee utasikia ritatoa kama ireee dokta anakunywa varuuu...aisee ire ni kariiii"

aaf ananiinamia ananambia "ivi pare uriwazaga nini jembe"?
sasa mm si unajua nina mastress yangu naona kama anazingua ivi ananirushia...ila ili niende nao sawa inabidi nimjibu...hhhahahahhahahah
!!

Jamaa mwingine mara achungulie nje anamuona barnaba kaunta akiongea na maaskari...anamwambia

" wee banaba wee njoo uwatoe wana apa, watarara hapa hawa ohooo!! aisee ira kabanaba ni kafupi jamani..."
yaani ikawa mwana anamix sana stori daah!! kucheka nataka huku nawaza mengi!!
aaaf unajua kuna zile mnakaa aaaf mnagonganisha macho mimi na mwanangu belle aaaf kama mnaongea kwa ishara ivi....daah!!!

Kuna mwana nakumbuka akanitazamaaaaa aaaf akasema
"ira riroma rinaonekana rijembe"

aliposema ivo belle kama naye akamtazama kwa kumkazia ivi uso wa mbuzi...basi mwana nikamsikia tena eti "iraa nyinyi nyote majembe tuuu"
hahahahha belle alinicheki aaf aka-smile ivii!!

nakumbuka vitu wlivokuwa wakisema mle ndani.....
"ira bere ire ngoma sijui masogange iree naikubariiii sana,
aaaf jamaa anaanza kuiimba, sasa akiimba utacheka aisee...

aaaf anaacha kuimba anasema " ira we dayamondi hakuwezi wewe...kisha wanaanza kubishana wao kwa wao"

Aisee mle ndani kuna watu wana majanga nyinyi daaah!! kuna wana yani unakuta sura nzima ana alama za mapanga tu humtazami mara 2, aaaf yeye anakukazia jicho tu kinoma noma!!...

Baadae kdg kuna mwarabu/msomali aliletwa na yeye..basi vile anaingizwa tu na lango kufungwa daah walimnyang'anyia kama mpira wa kona!! jamaa alipigwa ngumi/mateke fasta akavuliwa shati wakalizuia jamaa!! nikasema yeees, wana kweli sisi walituelewa kama hali zenyewe ndiyo hizi!!!
karibu mahabusu hiyo inaitwa!!!

"eti aisee roma nauza frash we ukitoka nitoe buku mbiri tu hii frash ina kirakitu ndani"........ hahaha sasa eti flash inauzwa aaf ina kila kitu sasa badala iwe empty yeye anasema ina kila kitu...

NWAYS yalitokea mengi sana mle ndani hadi tunaletewa msosi mchana, na wana wakatuzunguka wakisema tunawalinda mle kwa amani.. na tukaenjoy nao sana kuwa nao kwa muda ule wa masaa sio chini ya matano!!

Finally tulikuja toka kwa masharti...na kila kitu kikawekwa sawa....sasa baadae usiku tumetulia hotel na belle 9 ndio tunaanza kukumbushiana sasa story za kule..cheka sana...tukagonga macheers nini....ikabaki mumbukumbu tuu!!

Juzi nilikutana na mwana mmoja wapo (GEITA KWENYE SHOW)ni mwana mmoja kati ya wale tuliokuwa ndani siku hiyo!! TULICHEKA NA KUENJOY PAMOJA!!!

(PICHANI NI MASAA KADHAA BAADA YA KUWA HURU)!!

-Nikijaga kuyaimba haya kwenye ngoma zangu naambiwa NAKUSANYA HABARI ZA KITAIFA NA KIMICHEZO...HAHAHHAHAHAHHA
HAHH BONGO BANA!!!


"Wakati mwingine tunachukuliana poa ila tuna nguvu sana kwa mtaa/ tunapendwa sana/tuna face a lot of troubles"...bt we still
kip t real...ONE!!!

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates