TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA HELA NYINGI 2013

#2-Lady Jay Dee Huwezi amini,vuguvugu la Anaconda limemsaidia Jaydee si tu kukusanya mashabiki wengi zaidi,bali pia limempa fedha nyingi mno.Zaidi ya tiketi 3,500 zilinunuliwa kwenye show yake ya mwezi June ya Miaka 13 ya Muziki na kuingiza takribani shilingi milioni 100.Haikuishia hapo,albam yake Nothing But The Truth ilinunuliwa kwa kiasi kikubwa na kumfanya kuwa msanii pekee wa Bongo Flava anayeendelea kufurahia mauzo ya albam zake. Hits zake mbili,Joto Hasira na Yahaya kutoka kwenye albam yake hiyo,zimebadilisha maisha yake na kumfanya kuwa mwanamuziki mwenye show nyingi zaidi pia.Lady Jaydee ametumbuiza kwenye karibu show zote za Kili Music Tour ambako ameingiza shilingi milioni 25. Mwaka huu pia Lady Jaydee amefanya show nyingi kubwa ikiwemo ile ya uzinduzi wa filamu ya Lulu,Foolish Age,show yake kwenye Miss Tanzania 2013,Family Day Show ya Arusha iliyofanyika Eid Pili,Anaconda Show iliyofanyika Triple A na nyingine iliyofanyika Snow View Hotel. Akiwa Arusha pia,Lady Jaydee aliuza kopi za albam yake kama njugu pamoja na tiketi za Anaconda zilizouzwa kwa shilingi 15,000 kila moja. June mwaka huu pia,Lady Jaydee alitumbuiza kwenye semina ya kuwezesha wanawake kuondokana na njaa na umaskini,iliyofanyika chini ya mfuko wa fursa sawa kwa wote chini ya mama Anna Mkapa. Biashara yake ya Nyumbani Lounge,imeendelea kufanya vizuri pia kwa kupata wateja wengi wanaoenda kupata chakula,vinywaji na burudani kutoka kwa bendi yake ya Machozi. Bado anaingiza fedha kupitia udhamini wa Airtel kwenye show yake ya TV ya Diary of Lady Jaydee. Msanii huyo ambaye jina lake ni Judith Wambura pia miongoni mwa wasanii 24 wa bara la Afrika waliochukuliwa kwenye mradi wa Coke Studio Africa wa kampuni ya Cocacola unaoendelea jijini Nairobi Kenya.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates