TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA HELA NYINGI 2013 1-diamond platnumz

Hakuna ubishi kuwa,mwaka 2013 Diamond Platnumz ndiye msanii aliyeingiza fedha nyingi zaidi.Pesa nyingi ya Diamond imetokana na malipo ya show zake za ndani na nje ya nchi.Kwa uhakika,mwaka huu pekee,Diamond amefanikiwa kuingiza takriban shilingi bilioni 1. Kwa show za ndani peke yake,Diamond hutoza si chini ya shilingi milioni 10 ama 15 na kila wiki hufanya show zaidi ya 2.Hivyo tangu mwaka uanze,Diamond amekuwa akiingiza shilingi milioni 40 kila wiki.Tour za nje alizofanya mwaka huu ni pamoja na zile za Uingereza ambako alifanya show kwenye miji mitatu,show ya Burundi na Congo,show mbili za Kenya (Nairobi na Mombasa),show ya nchini Comoro ambako alilipwa si chini ya dola 30,000 na show ya Malaysia wiki iliyopita. Kwa upande wa show za hapa nyumbani ambazo ni nyingi mno zisizo na idadi,ukiachana na zile za kawaida,Diamond aliingiza shilingi milioni 40 kwenye show 4 za Kili Music Tour ambapo kila show alilipwa shilingi milioni 10.Ndiye msanii aliyelipwa fedha nyingi zaidi kwenye ziara hiyo. Pia amefanya show kadhaa za Fiesta 2013,show za promotion za Tigo na makampuni mengine Tamasha la Matumaini,show ya Tulizana Tuko Wangapi ya Leaders Club,show yake na Nay wa Mitego (Dar Live na Maisha Club). Mwezi February 16 mwaka huu, Diamond alifanya show jijini Arusha ambayo kiingilio chake kilikuwa ni shilingi 150,000 ndani ya Club Safari na ukumbi kufurika. Miezi kadhaa iliyopita pia hitmaker huyo wa ‘Number 1’ ameshaalikiwa kwenye show corporate kuburudisha wafanyakazi wa benki na taasisi zingine pamoja na watu binafsi na zote hizo zimemuingizia fedha nyingi. Pamoja na show,Diamond amekuwa akiingiza fedha nyingi zaidi kwenye malipo ya ringtones ambapo kila baada ya miezi mitatu amekuwa akiingiza si chini ya shilingi milioni 20.Kwa mujibu wa Push Mobile,akaunti ya Diamond kwenye kampuni hiyo ndio inayoingiza fedha nyingi kuliko msanii mwingine yeyote wa Bongo Flava. Mkataba exclusive alioingia na kampuni ya simu ya Vodacom kuuza wimbo wake mpya My Number One kama muito wa simu, umezidi kumpandisha juu na ikidaiwa kuwa mkataba huo ni wa mamilioni ya shilingi. Ikumbukwe pia,Diamond ni balozi wa Cocacola. Mkataba huo ambao haijajulikana umemuingizia shilingi ngapi,lakini ni fedha inayoweza kuwa si chini ya shilingi milioni 100. Diamond ni miongoni mwa wasanii wengine 23 wa Afrika akiwemo Lady Jaydee kwenye mradi mkubwa wa Cocacola wa Coke Studio africa.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates