TOP 10 YA WASANII WA BONGO FLAVA WALIOINGIZA HELA NYINGI 2013 4-Ommy Dimpoz

Ommy Dimpoz ambaye kwa sasa yupo kwenye ziara ya muziki nchini Marekani ameingiza fedha zake nyingi kupitia show alizofanya. Ziara zake za Ulaya na Marekani pekee zimemuingizia dola 50,000 ambazo ni sawa shilingi milioni 81. Tangu aachie wimbo wake mpya Tupogo,tayari Ommy ameshaingiza shilingi milioni 50.Kwenye show yake ya hivi karibuni ya Tupogo Night iliyofanyika Club Billicanas,Ommy alipeleka nyumbani shilingi milioni 10 baada ya kukata gharama zote.Watu 1,770 walihudhuria show hiyo. Show yake ya Burundi ya mwanzoni mwa mwezi uliopita ilimuingizia staa huyo shilingi milioni 30. Ommy hutoza si chini ya shilingi milioni 7 kwa show na kwa mwezi,amekuwa na uhakika wa kufanya show tatu ama nne za ndani bila kusahau show za Kili Music Tour. Hivi karibuni kwenye segment ya Tell it All ya Bongo5,Ommy alifunguka kuwa makampuni mengi yamekuwa yakimfuata kumpa endorsements lakini msimamo wake wa kutaka kulipwa fedha ya uhakika imemfanya azikatae nyingi lakini yupo mbioni kupata deal kubwa. Mpaka sasa Ommy anajenga nyumba mbili kwa mpigo zenye thamani ya shilingi milioni 250 hadi zilipofikia. Tayari ana viwanja vingine viwili anavyotaka kuangusha mijengo mingine.Hivi karibuni pia atakuja na clothing line yake ya PKP.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates