Baada ya Irene Uwoya kuweka kituko cha aina yake jana, soma hiki kingine tulichokipata leo


Baada ya Irene Uwoya kuweka kituko cha aina yake jana, soma hiki kingine tulichokipata leo
Jana mwanadada Irene Uwoya aliwavunja mbavu wadau mbalimbali wa filamu nchini baada ya kuweka picha (Inayoonekana pichani)  ya moja ya scenes za filamu yake mpya ambayo bado hatujapata jina lake ikumuonesha jambazi  (aliyepewa jina la “JAMBAZI MSTAARABU” na fans wa filamu )akimtishia Irene Uwoya bastola kama anataka
kumuua hivi.
Jambazi huyo ambaye kwanza anaonekana “Sharobaro” na akifanya uhalifu kistaarabu kwa kuvua viatu “eti asije akachafua nyumba anayoiba” huku wananchi wengine wakiongezea kuwa Jambaz ana mzuka wa kuiba mpaka viatu kavua,
Baada ya picha hiyo kupondwa sana na wadau leo hii mdau wetu mmoja  ameamua kututumia kioja kingine alichowahi kukutano nacho kwenye filamu zetu hizi za bongo.
Mdau anasema japokuwa hakumbuki jina la filamu hiyo vizuri anakumbuka scene moja ya kwenye filamu hiyo ambayo kulikuwa na jini mmoja aliyetumwa akamuue dada mmoja katika filamu hiyo.
Haya chini ndio maneno ya mdau wetu huyu, yote hii ni katika kuboresha filamu zetu na sio kuziponda.
“Kuna cku nlikua home siriaz nacheki Bongo muvi... Nmevumilia kinoma najifanya mzalendo... Sasa filamu ilikua ina jini moja katili sana... Limetumwa likamuue maza mmoja na ndugu... Sasa likawa linavuka bara bara eti...taratibu nikaona linajisogeza kwenye zebra cross  huku likiangalia kushoto na kulia before halijavuka..jini gani sasa hili? Sio kwamba linatakiwa livuke tuu? Mi sijawai kusikia jinni likiogopa kugongwa na gari.. .Nlimind sana..”
Dah, kwa mwendo huu itabidi tujipange sana yani, ni hayo tuu!
USHAURI: Tujaribu kutengeneza uhusika halisi ndani ya filamu sio bora liende.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates