Msanii Shaa Atia Saini Mkatamba Mpya Na Saidi Fella. Fuatilia Hapa


Msanii wa kike kutoka Tanzania mwenye uwezo mkubwa wa kufanya muziki  wowote 'Shaa' ametia wino kwenye mkataba wa miezi sita na Saidi Fella kupitia Mkubwa Na Wanawe. Saidi Fella amesema leo kupitia sammisago.com kuwa mkataba huu ni wa muda mfupi na watafanya kazi tofauti na Shaa sababu anauwezo mkubwa wa kuimba na kufundisha muziki.

Saidi Fella amesema wamefanya mazungumzo na Aliyekuwa manager wa Shaa 'Master J' na wamekubaliana kuwa atafanya kazi na mkubwa na wanawe kwa misingi yao na baraka zote wamepewa.

Bab Tale amekuwa akifanya kazi na Shaa kwa muda sasa na kuhamia kwa Said Fella kuta msaidi zaidi Shaa kuteka soko la nyumbani zaidi. Shaa amekuwa moja ya  wasanii Kutoka Tanzania mwenye mashabiki wengi nje ya nchi yake.

Awali Shaa aliwahi kufanya kasimamiwa na  Ay Na Master J. I Hope hizi ngoma mbili kutoka kwa Shaa zitatisha sana hapa Tanzania, Moja amefanya na At na Nyingine Na Rapper Shetta.

Shaa amesema haya ni maamuzi mazuri na yataongeza sana mashabiki wa muziki wake Nyumbani

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates