Simba Wawaongoza Yanga katika "Nani Mtani Jembe?

Pamoja na mchezo wa watani wa jadi kuisha kwa sare ya 3-3 Jumapili ya wiki iliyopita, Simba wameanza kuongoza katika kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inayoendelea hivi sasa kwa kuwashirikisha mashabiki wa klabu hizi mbili kongwe nchini.

Mpaka sasa Simba wana kitita cha Shilingi 50,012,500.00 wakati watani wao wa jadi Yanga wana Shilingi 49,987,500.00. Upigaji wa kura katika kampeni hii unahusisha mashabiki kununua Bia ya Kilimanjaro na kusoma namba zilizo chini ya kizibo na kutuma kwa ujumbe wa simu wakianza na jina la timu wanayoishabikia kwenda 15440 na moja kwa moja Shilingi 1,000 kupunguzwa kutoka kwa wapinzani na kuwekwa kwa timu yao. Matokeo ya Nani Mtani Jembe yanapatikana katika tovuti ya http://kilitime.co.tz/campaigns/nmj/
 
Kampeni ya "Nani Mtani Jembe?" inaendeshwa na Kilimanjaro Premium Lager ambao ni wadhamini wakuu wa klabu za Yanga na Simba

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates