Babu Seya na Mwanaye Papii Kocha Kuendelea Kutumikia Kifungo cha Maisha, Rufaa Yao Yatupiliwa Mbali

Papii na Babu Seya
Hukumu ya rufaa ya mwanamuziki Nguza Viking na mwanaye Nguza Johnson 'Papii Kocha' imewarejesha tena jela kuendelea kutumikia kifungo cha maisha mara baada ya hoja za serikali kiushahidi kuzishinda zile za upande wa utetezi.

Mnamo mwaka 2004 Babu Seya na Papii Kocha walihukumiwa kifungo cha maisha jela baada ya kupatikana na hatia ya kuwanajisi watoto wa Shule ya Msingi, Mashujaa, Sinza jijini Dar.

Wamekuwa wakikata rufaa mara kwa mara lakini zimekuwa zikigonga mwamba na kwa mujibu wa taarifa inasemwa kwamba hukumu ya rufaa hii ndiyo ya mwisho kusikilizwa.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates