BABY MADAHA CHUPUCHUPU KUBAKWA HUKO MOMBASA.

 
STAA wa filamu na muziki Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’ amenusurika kubakwa na vijana wa kihuni nchini Kenya maarufu kama machokoraa.

Tukio hilo lilitokea hivi karibuni pande za Mombasa nchini Kenya wakati nyota huyo alipokuwa akirekodi video ya wimbo wake uitwao The Gal Bladder ambapo vijana hao walikatisha shughuli nzima na kuanza kumkimbiza Baby Madaha.


“Daah! Ilikuwa noma, ilikuwa usiku sasa wakati meneja wangu akinielekeza matakwa ya video hiyo ambayo yalihitaji vijana wa mtaani, ghafla wakatokea vijana wenyewe wa mtaani na kutaka kunibaka. Bahati nzuri nilifanikiwa kutimua mbio na kuwazidi,” alisema B.


Credit:zotekaliblog.com

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates