SAKATA LA KINGWENDU KUMTAPELI MR BONDI STORY NZIMA IKO HAPA!!


Mr Bondi aliskika hivi karibuni akizungumza kwa njia ya simu katika Radio moja hapa jijini Dar esa Salaam akimlaumu Vikali Msanii Mwenzake

Kingwendu kumtapeli shilingi Laki 2 alizompa kama advance ya Kufanya shooting ya Move yao Mpya ambayo  Wamo Mastaa kibao akiwemo Yeye Mr Bondi,Natasha,Monalisa na Wengine Kibao.

Alichokifanya Kingwendu ni kutoonekana siku ya kufanya hiyo filamu na kuzima simu zake kwa siku sita bila taarifa yeyote na mbaya zaidi alimdanganya Mr Bondi kuwa mama yake anaumwa hivyo anaenda kumwona ila atawaikurudi kabla ya siku ya shooting.

Taarifa zaidi ni kwamba Kingwendu alipata show nchini Msumbiji.Baada ya kupata tetesi hizi ilibidi babamzazi.com imtafute Kingwendu ili kujua ukweli.

Alikiri ni kweli Mr Bondi alimpa laki 2 kama advance na alikuwa Tayari kufanya hiyo kazi ila kwa Bahati nzuri alipata show Msumbiji na walompa show walimdanganya kuwa wamemkatia tiketi ya ndege ya go and return hivyo alijua angewai.

Mbaya zaidi alipofika kule ikawa shida kurudi baada ya kukosa ndege.Hivyo ilibidi asubiri Ndege.

Hata hivyo amemuomba radhi Mr Bondi kwa kitendo alichokifanya na Anamuomba amsamehe sana yeye ni Binadamu na kilichomponza ni Ndege,alijua angewai.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates