KAMA ULIPITWA,HAYA NDIO MAJANGA MENGINE YA MAANDALIZI YA KOMBE LA DUNIA HUKO BRAZIL 2014

majnga brazil 1
Maandalizi ya mashindano ya kombe la dunia yako hatarini kuingia dosari baada ya wafanyakazi wa viwanja kadhaa ambavyo vinaendelea kujengwa kupanga kufanya mgomo .
Wafanyakazi hao wamepanga kufanya mgomo baada ya kutoridhishwa na mazingira ya usalama kwenye maeneo ya ujenzi .
majanga brazil 2
Wafanyakazi hao wamekuwa wakilalamikia hali ya usalama kuwa mdogo kwenye viwanja ambavyo ujenzi wake haujakamilika baada ya kuwepo na matukio ya wafanyakazi kufariki dunia kwenye maeneo ya kazi kutokana na ajali katika matukio tofauti  .
Endapo mgomo huo utafanyika maandalizi ya kombe la dunia yatakuwa yamepata pigo kutokana na baadhi ya viwanja kushindwa kukamilisha ujenzi wake ndani ya muda uliopangwa.
majanga brazil 3

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates