WANAWAKE 16 WAPANDISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA KUCHEZA WAKIWA UCHI

WANAWAKE 16, walishtakiwa Jumatatu katika mahakama ya Kibera kwa kupatikana wakisakata densi wakiwa uchi katika kilabu kimoja cha usiku jijini Nairobi mwishoni mwa wiki.
Mahakama ilifahamishwa kwamba wanawake hao wa umri wa kati ya miaka 18 na 24 walikamatwa katika kilabu cha Barrels mtaani Langata jijini Nairobi Jumamosi usiku wakishiriki kitendo cha aibu kwa kuvua nguo katika eneo la umma na kusakata densi
Kulingana na shtaka, wanawake hao walitenda kosa hilo kwa nia ya kujipatia fedha  kupitia kitendo cha aibu jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

Ilidaiwa kwamba polisi walienda katika kilabu hicho baada ya kupashwa habari na umma kwamba kundi la wasichana lilikuwa likishiriki kitendo hicho na kuwakamata wasichana hao.

Hata hivyo walipofikishwa mbele ya Hakimu Mkazi wa Kibera Bw Aswani Opande aliagiza wasishtakiwe katika kesi moja.

Alirudisha karatasi ya mashtaka kwa polisi na kuwaagiza wawashtaki katika makundi mawili ili mahakama iwe na kazi rahisi ya kushughulikia kesi hiyo.

Katika kesi nyingine, Bw Aswani alimwachilia mwanamume walioshtakiwa kwa kupanda gari lililobeba abiria kupita kiasi akisema dereva na makanga wake wangeshtakiwa pia.Alisema ni makosa kuwashtaki abiria na kukosa kuwashtaki wahudumu wa magari yanayowabeba

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates