AUDIO - SIKILIZA GUMZO LA RAMADHANI NA UJIFENZE MENGI KUHUSU MWEZI HUU MTUKUFUKARIBU SANA KATIKA GUMZO LA RAMADHANI,ALHAMDULILLAH TUNAKUTANA TENA KATIKA MFUNGO  MWENGINE WA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI,TUKITEKELEZA IBADA YA SWAUM AMBAYO NI NGUZO YA NNE KATIKA NGUZO 5 ZA DINI YA KIISLAM.

MSIKILIZAJI,BILA SHAKA MWEZI HUU MTUKUFU UNA HADHI NA HESHIMA YA KIPEKEE SANA KUTOKANA NA FADHILA KUBWA WANAZOPATA WAUMINI WANAOTEKELEZA IBADA HII YA SWAUM.
HIVYO KUNA MENGI HUFANYIKA TOKEA KUINGIA KWAKE KATIKA KUUPOKEA HADI TUNAPOUAGA.
LICHA YA WENGI WETU KUFAHAM YOTE HAYO,KUNA MABADILIKO MAKUBWA YANAYOONEKANA KATIKA JAMII YETU HUSUSAN KWA VIJANA KATIKA SUALA LA STARA NA STAHA YA MWEZI HUU HALI AMBAYO INALETA MASWALI MENGI SANA YA NINI KIMEJIRI MPAKA BAADHI YA WATU WANASHINDWA KUUSTAHI MWEZI HUU?
NINI KIMEWASIBU? AMA HAWAFAHAMU JINSI VISIWA HIVI VYA UNGUJA NA PEMBA VILIVYOKUWA NI KIMBILIO LA WAGENI WENGI KUJA KUFUNGA ILI KUTEKELZA IBADA HII BILA YA VIKWAZO VYOYOTE KWA KUWA ZANZIBAR IKISIFIWA KOTE ULIMWENGUNI KUTOKANA NA WAKAAZI WAKE WALIVYOKUWA WAKIACHA YAO YOTE KWA HESHIMA YA MWEZI HUU MTUKUFU?
MABADILIKO HAYO NI KOTE MIJINI NA HATA VIJIJINI NA NDIO MAANA  LEO GUMZO LA RAMADHAN LIMEFIKA KATIKA KIJIJI CHA BWEJUU MKOA KUSINI UNGUJA,UMBALI WA MAILI 32 KUTOKA UNGUJA MJINI ILI KUWEZA KUNG’AMUA KUNAAANI?!!!
NA HUYU NI BIBI MARYAM ALI HASSAN AMBAE NI MAMA WA MAKAMO MKAAZI WA BWEJUU AKIELEZA
BWEJUU NI MIONGONI MWA VIJIJI VILIVYOBARIKIWA FUKWE NZURI NA SAFI ZA BAHARI YA HINDI,HALI INAYOWABURUDISHA WAKAAZI WA ENEO HILI KWA UPEPO MWANANA.
KIJANA JUMA MUSSA MKALI NAE NI MZALIWA KATIKA KIJIJI HIKI,NA HAPA ANATUELEZA ANAYOYAFAHAMU KATIKA KUMBUKUMBU ZA MAKUZI YAKE KATIKA KIJIJI HIKI CHA BWEJUU
LAKINI ILI KUFAHAM UTANDU NA UKOKO  WA HISTORIA YA HAPA BWEJUU KATIKA MWEZI WA RAMADHANI,NIMEBAHATIKA KUZUNGUMZA NA MZEE ALI HASSAN MAJAALIWA AMBAE NI MZALIWA NA AMETUMIA UJANA WAKE WOTE MPAKA KUFIKIA UZEE BADO AKIWA NI MKAAZI WA BEJUU.
KWA KUMALIZIA NIKAELEKEA NYUMBANI KWA BIBI MTUMWA NASSOR HAJI AMBAE HAKUSITA KUNIELEZA ANAVYOIKUMBUKA BWEJUU YA ZAMA ZAKE KATIKA MFUNGO WA MWEZI MTUKUFU WA RAMADHANI.
NAAM MSIKILIZAJI,NI DHAHIRI KWAMBA TUMEPOTEZA MWENENDO MZURI WA MAISHA AMBAO WAZEE WETU HAPO KABLA WALIKUWA WAKIUFUATA NA NDIO ULIOWAWEZESHA WAO KUISHI KWA UPENDO NA KUSAIDIANA.
BADO HATUJACHELEWA,TUKIAMUA KWA PAMOJA TUNAWEZA KURUDISHA TARATIBU NZURI ZENYE MAADILI KATIKA MWEZI HUU MTUKUFU WA RAMADHANI NA HATA KATIKA SIKU ZA KAWAIDA.
KUTOKA HAPA BWEJUU.MKOA WA KUSINI UNGUJA ULIKUWA NAMI MULHAT YUSSUF SAID NIKITAKIA SWAUM NJEMA NA RAMADHAAN KAREEM.
sililiza full interview hapa 


Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates