NEWS - TETESI ZA SOKA ULAYA


Arsenal watatakiwa kutoa pauni milioni 24 kumsajili kiungo wa Sporting Lisbon William Carvalho, 22 (Daily Telegraph), beki wa Southampton Dejan Lovren, 25, anakaribia kukamilisha uhamisho wa pauni milioni 20 kwenda Liverpool wiki hii (Times), Liverpool wamemuulizia kiungo wa Real Madrid, Isco, 22, baada ya mabingwa hao wa Ulaya kumsajili Toni Kroos na James Rodriguez kutoka Colombia (Daily Star), Leicester wanamfuatilia mshambuliaji kutoka Algeria Islam Slimani, 26, anayechezea Sporting Lisbon (Daily Mail),

beki wa Manchester City Micah Richards, 26, anataka kwenda kucheza kwa mkopo baada ya Tottenham, Newcastle na Liverpool kukataa kutoa pauni milioni 7 (Daily Express), mshambuliaji Didier Drogba, 36, anakaribia kurejea Chelsea wakati mazungumzo kuhusu mkataba wa mwaka mmoja yakiendelea (Daily Mail), Tottenham watamfuatilia kiungo Morgan Schneiderlin, 24, mara baada ya kukamilisha usajili wa beki wa kushoto wa Swansea Ben Davies, 21 (Daily Mirror), kuwasili kwa Davies Tottenham kutafungua njia kwa Danny Rose kuhamia Hull City kwa pauni milioni 6 (Sun), winga wa Chelsea Mohamed Salah, 22, atasafiri na timu yake kwenda Austria kwa mechi za kabla ya kuanza msimu licha ya wasiwasi wa kutakiwa kuhudhuria mafunzo ya kijeshi Misri (Daily Telegraph), mkurugenzi mkuu wa AC Milan Adriano Galliani amekanusha kupokea dau lolote kutoka Arsenal kuhusiana na Mario Balotelli (Sky Sports), Arsenal wamefikia makubaliano ya pauni milioni 3.2 ya kumsajili kipa David Ospina , 25, kutoka Nice (Le Figaro), Real Madrid wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester City Alvaro Negredo, 28, kuziba nafasi ya Alvaro Morata anayekwenda Juventus (Marca), Chelsea wametoa pauni milioni 20 kutaka kumsajili beki Miranda , 29, kutoka Atlètico Madrid (AS.com), meneja wa Napoli Rafael Benitez anataka kumsajili Christoph Kramer, 23, kutoka Borussia Moenchengladbach (L'Equipe),

 Bayern Munich wapo tayari kutoa pauni milioni 33 kuwazidi kete Barcelona kumsajili Juan Cuadrado, 26, kutoka Fiorentina (Bild), Paris St-Germain huenda wakashindwa kumsajili Paul Pogba, 21, kutokana na sheria za matumizi ya fedha. Hali hiyo inatoa mwanya kwa Real Madrid na Manchester United zinazotaka kumsajili (Lefigaro) hatma ya Xherdan Shaqiri haifahamiki baada ya mazungumzo ya kuhamia Liverpool kukwama. Kiungo huyo wa Bayern Munich pia anasakwa na AS Roma na Juventus (Bild) Atlètico Madrid wako makini kumsajili tena Fernando Torres na wameanza mazungumzo ya kutaka kutoa pauni milioni 12.6 (Eurosport), matumaini ya Arsenal na Chelsea ya kumsajili Sami Khedira huenda yakawa yamepata pigo baada ya Real Madrid kuwapa Monaco mchezaji huyo atakayenunuliwa kwa takriban pauni milioni 20 (Daily Mirror).


Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates