NEWS - VAN GAAL AELEZA SABABU ZA KUBADILI KIPA JANA

Kocha wa Uholanzi Luis van Gaal amesema urefu wa kipa Tim Krul ndio ulimfanya amchezeshe katika mikwaju ya penati katika mchezo wa robo fainali dhidi ya Costa Rica.

Krul, mwenye urefu wa futi 6 na inchi 4, (mita 1 sentimita 93) aliingia badala ya kipa aliyeanza Jasper Cillessen zikiwa zimesalia sekunde chache kabla ya mikwaju ya penati kuanza kupigwa. Jasper ana urefu wa futi 6 inchi 2 (Mita1 sentimia 87).
Krul aliweza kupangua penati mbili, na hivyo Uholanzi kushinda kwa magoli 4-3.
"Tulidhani kuwa TIm ndio kipa bora wa kuzuia penati," alisema Van Gaal. "Ni mrefu na ana nafasi zaidi ya kuzuia."
Menenja huyo wa Manchester United aliongeza kusema: "Ilifanikiwa, ilienda vyema. Ninajivunia kidogo kwa hilo."
Uholanzi, timu pekee kati ya nne zilizosalia ambayo haijawahi kushinda Kombe la Dunia, itapambana na Argentina mjini Sao Paulo siku ya Jumatano. Brazil itacheza na Ujerumani katika nusu fainali ya kwanza siku ya Jumanne.

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates