Na Joseph Muhozi 'Josefly', Mtangazaji Victoria fm Musoma, Rapper
Kama Tanzania tunaweka kumbukumbu ya nyimbo zilizowahi kuhit ama zinazohit zaidi basi nyimbo za mapenzi zitachukuwa 75% kwa makadilio ya chini.
Kama Tanzania tunaweka kumbukumbu ya nyimbo zilizowahi kuhit ama zinazohit zaidi basi nyimbo za mapenzi zitachukuwa 75% kwa makadilio ya chini.
Lakini pia tukiangalia hata album za
wasanii wanaoimba ambao ndio wanaongoza kwa kuimba nyimbo hizi basi wengi wao
album zao zinabeba 90% love songs.
Lakini Sikuwahi kufikiria kama kuna Rapper
(MC) wa TZ tena anaejiita ‘Hip Hop’ anaweza kurekodi album ama mixtape yenye
nyimbo zote za mapenzi!! No, sikuwahi….nadhani wewe pia hukufikiria hilo,
lakini AZMA ndiye aliweza kunibadili fikra baada ya kutangaza kutoa mixtape
yenye nyimbo 15 ambazo zote ni za mapenzi.
Inawezekana kabisa jina ‘AZMA’ sio jina
linalofahamika kwa watu wengi kama majina ya mastaa wengine, lakini naweza
kusema katika uandishi na idea ‘ni dhahabu mchangani sema tu hajashtukiwa’.
Jina lake halisi ni AZMA MPONDA.Nilianza
kumsikia AZMA nilipodownload wimbo wake unaoitwa ‘Bongo flava inakufa’, labda
jina la wimbo na idea zilivuta zaidi kusikia imekuwaje. Mashairi yaliyokuwemo
yana maneno makali kidogo akiwarushia bomu aliowaita bongo fleva na bongo fleva
yenyewe, lakini alitoa sababu na mifano inayotoa picha ya kile kinachofanyika
kweli, Ni wimbo unaofaa kukaa kwenye mixtape.
Hapo nikajikuta nakuwa mfuasi wa nyimbo
zake taratibu na nikaunasa wimbo mwingine na kuudownload unaitwa ‘My name is
Hip Hop’. Kiukweli nilipata ladha ya Hip Hop kweli na nikabaki na chorus
kichwani “my name is Hip-, My father is Hop, I go by the name of Hip- Hop”.
Nikazidi kumfatilia taratibu kwa hili jina
‘AZMA MPONDA, UMABE’, nikamsikia kwenye nyimbo nyingine za watu kama ‘Saa
mbovu’ aliyofanya na Nash Mc, Young Killer na Stereo, ‘Connection’ aliyofanya
na Ezden na wengine na nyingine nyingi, baadae nikamsikia amejiunga na familia
ya Tamaduni Music, nikaona hapo panamfaa huyu jamaa kwa sababu ni karakana ya
Rhymes ataiva zaidi. Lakini nikampigia
salute tena nilipomuona kwenye Fid Friday Freestyle ya Mwanza nikakubali kweli
ameiva.
Nakumbuka niliwahi kumualika mwaka jana
kwenye show niliyokuwa naifaya Radio SAUT inayoitwa ‘HIP HOP 120’, na baada ya
show nilimpigia salute kihip hop. Jamaa ni mkali.
Kwa jinsi nilivyokuwa namfahamu sikuwahi
kuwaza kuwa ipo siku ntamsikia akiconcentrate kwenye love songs, lakini naweza
kusema alinibadili mawazo na ndiye msanii pekee wa Hip Hop TZ niliyewahi
kumsikia mimi amefanya album yenye nyimbo 15 zote za mapenzi, ama hata mixtape.
Kikubwa zaidi sio tu kutoa nyimbo nyingi za
mapenzi, lakini kinachonishika zaidi ni uandishi wake wa hizo nyimbo za
mapenzi.
Kipimo cha penzi ndio wimbo wa kwanza
kutoka kwenye mixtape yake aliyoipa jina la LOVE STORIES.
Nilipousikiliza wimbo huu kwa mara ya
kwanza tu niliurudia mara tatu, na hata nilipoucheza redioni (Victoria fm)
wasikilizaji walikuwa wanatuma message wakiyarudia yale waliyoyasikia kwenye
huu wimbo, na kuomba niucheze tena.
Kwa kweli huu ni utunzi ambao wasanii wengi
inabidi kuuchukuwa kama mfano, ili kuishinda ile statement ‘kila siku mapenzi
tu’, kwa sababu mapenzi yanatopic nyingi sana ambazo zinaweza kumfanya mtu
ahisi anasikiliza ujumbe unaomhusu hata kama sio mfuasi wa mapenzi kiivo.
AZMA ameweza kuyazungumzia mapenzi kwa
kujitoa yeye kabisa na sio kumuimbia girlfriend wake wala story ya mshikaji
wake aliyetendwa, wala kuyalaumu mapenzi kwa sababu ya dhiki zake na kuachwa.
Lakini ameweza kugusa angle tofauti tofauti kwa style ya kuuliza ni nini kipimo
cha penzi? Na ukimsikiliza lazima utapata kitu cha kutafakari, kwa sababu kila
kitu kimekuwa covered kwenye verse tatu ambazo zote hazilegilegi.
Ni kama anaongea na wewe, lakini pia ni
kama anamwambia yule, wakati huo huo anaingia nae kidogo kwenye wimbo wake.
Lakini kila angle anauliza hili swali nini kipimo cha penzi? Kweli Wengine
wanalia, wengine wanacheka, na wanaocheka wanaweza kuwa waliaji watarajiwa and
vise versa. So nini kipimo cha Penzi??
Mpangilio wa verse na mashairi mazito
lakini mepesi kueleweka yanaweza kukupa picha ya maswali mengi yanayohusu
mapenzi, na mikasa ya mapenzi na mwisho utajikuta unajiuliza ni nini kipimo cha
penzi la kweli.
Ni vigumu sana kukosa mfano wako kwenye
haya mashairi, hata kama sio direct basi kuna mstari utakugusa indirect.
Wimbo huu ni mfano wa kuigwa kwa wasanii
wengi hasa wa Hip Hop ambao wengi wao wanazichukulia poa nyimbo za
mapenzi…lakini pia kwa waimbaji wanaoandika idea zinazofanana kila
siku,…mapenzi yanaweza kuwa na uwanja mpana na yakahusisha mpaka siasa,
historia, uchumi, afya, psychology, mazingira n.k. Yap hata mazingira, kama
huamini basi soma kitabu cha DR.Msafiri, title nimesahau kidogo ila ni cha
mazingira utaona jinsi mapenzi yakigeuzwa kuwa ngono yanavyoweza kuchafua
mazingira, so hiyo pia ni idea.
Sasa kama ni hivi kweli unaweza kuona jinsi
gani mapenzi yakiandikiwa mashairi
mazuri hayawezi kuisha wala kuboa hata kidogo, kwa sababu in every aspect of
life mapenzi yamepenya.
Big Up sana AZMA MPONDA I really appreciate
your work, na ambae hajakufahamu vizuri namualika aitafute na kuisikiliza hii
mixtape ya LOVE STORIES.
Post a Comment