Oprah Winfrey |
List ya wanawake wanaojihusisha na entertainment
wanaolipwa mpunga mrefu zaidi duniani kwa ajili ya kazi zao kwa mwaka
iliyotolewa na Forbes inaonesha kuwa Oprah Winfrey anayeendesha talk show
anashikilia nafasi ya kwanza, ambapo kati ya may 2011 na may 2012 amepokea $
165 million. Na imegundulika kuwa bado kuna mshahara mwingine hajapata, kwa
hiyo hautajumuishwa kwenye pato la mwaka ujao, 2013 ili isiwe nafasi ya
kumuongezea ushindi tena mwaka ujao kumbe kuna pato la mwaka huu bado
analisubiria.
Britney Spears |
Katika list hiyo nafasi ya pili imekamatwa
na judge wa X Factor mwanadada Britney Spears, ambae yeye ameingiza mpunga wa
ukweli kiasi cha $58 million ndani ya mwaka mmoja. Kwa mujibu wa Forbes Spears
alimake mkwanja mrefu sana kupitia album yake na hasa kupitia tour ya album hiyo
aliyoibatiza “Femme Fatale tour”, na
alijazilishia kwa mkataba mnono wa kuendesha X Factor ambao ni $15
alizozisign.
Taylor Swift |
Nafasi ya tatu imekamatwa na mwanadada
Taylor Swift ambae ana historia ya aina yake na MTV VMAs, alipovamiwa jukwaani
na Kanye West, na hili tukio liliwafanya watu wengi zaidi kutega masikio kwa
huyu mwanadada mwenye umri wa miaka 22 hivi. Yeye amemfata kwa karibu sana
Briteney Spears kwa kuingiza $57 millioni kwa mwaka kama pato halisi. Huyu ni
mwanadada mwenye umri mdogo zaidi kwenye hii list na tour yake ya Speak Now
ilichangia kwa kiasi kikubwa sana pato lake lakini pia ngoma kibao kali
alizoachia ikiwemo ile safe &sound. Na mwezi huu anatarajia kuachia album
yake inayoitwa Red. Kumbuka wimbo wake wa kwanza ulikaa kwenye nafasi za juu sana
za Billboard’s Hot 100 chart kwa muda wa wiki tatu.
Rihanna |
Nafasi ya nne imekamatwa na the R&B
Queen Rihanna, lakini hapa amefungana na mwanadada Ellen DeGeneres wote wakiwa
wameingiza kiasi cha $53 million.
Nafasi ya tano imekatwa na Lady Gaga
na jaji wa zamani wa American pop Idol
Jeniffer Lopez, wakali hawa wamefungana pia na wameingiza mpunga kiasi cha $52
million kwa kipindi cha mwaka mmoja. Gaga album yake iliyoambatana na tour ya
Born This Way imemsaidia kufika hapo.
Wakati majina yanaendelea kushuka, list
ilifungwa na supper modal Gisele Bundchen ($45 million) Katy Perry ($45
million) na Judge Judy wa TV show ($45 million).
Post a Comment