Nick Minaj |
Wiki chache baada ya Mariah Carey kukanusha
tetesi kuwa alikuwa na beef na Young Money Queen Nick Minaj ambae ni jaji
mwenzake kwenye American Idol sasa mambo yamekuwa tofauti baada ya video yenye
picha tofauti kabisa na kile kilichoelezwa na Carey kusambaa kwenye mitandao.
Video hiyo inaonesha Nick Minaj akiwa
kakasirika na anampa makavu live Mariah Carey, tukio hili limetokea wakati
wanaendelea na kazi yao ya kujaji washiriki mbalimbali na safari hii walikuwa
Charlotte, North Carolina.
Mtu mmoja ambae alishuhudia live tukio hilo
amesema kuwa Nick Minaj alionekana kupandisha mzuka na kufikia hatua ya
kumtishia the R&B diva Mariah Carey na kusema “I’m gonna knock you out”.
Chanzo hicho kiliendelea kusema kuwa Nick
Minaj aliongea kwa sauti ya juu sana na kumtolea matusi makali Mariah Carey
akisema “I told them, I’m not f***kin’
putting her f**kin’ highness there.” Lakini hii sehemu haikushikwa na lensi ya
camera hiyo iliyokuwa inachukua matukio ya American Idol.
Inasemekana kuwa hii varangati ilitokea
baada ya kutofoutiana sana katika maamuzi kwa washiriki walio-perform siku
hiyo. Wakati hayo yanatokea, Nick Minaj na Mariah Carey walikuwa wamekaa kwenye
meza ya majaji, na jaji mwenzao Keith akiwa amekaa katikati yao na Randy
Jackson akiwa amekaa mwishoni upande wa Mariah Carey.
Kutokana na hali hiyo watayarishaji wa
American Idol iliwalazimu kusimamisha performance ya siku hiyo ili majaji hawa
wacool down kwanza. Hali hii inaonekana kuwatishia waandaji wa American Idol na
wana wasiwasi kama Nick Minaj na Mariah Carey watadumu kwa muda mrefu wakiwa
wanafanya kazi yao pamoja kama majaji wa American Idol.
Mariah Carey |
Katikati ya mwezi September iliripotiwa
kuwa Nick Minaj na Mariah Carey hawana maelewano mazuri, na mtu mmoja ambae ni
mfatiliaji wa mambo ya muziki Marekani alisema hata Mariah Carey alipopigiwa
simu kuambiwa kuwa Nick Minaj ndo atakuwa jaji mwenzake kati ya wale wanne
alikata simu.
Lakini September 17 ambapo MTV ilienda New
York pale ambapo American Idol ilikuwa imeanza na ikafanyika kwa siku mbili,
ili kujionea nini kilikuwa kinaendelea kati ya Mariah Carey na Nick Minaj, na
walipouliza kuhusu kutoelewana, wote walikuwa wanatabasamu kama vile walisikia
utani hivi, na Mariah Carey akaonesha kushangazwa na taarifa hizi jinsi
zilivyosambaa kwa haraka ndani ya muda mfupi sana, na akamaliza kwa kusema
"It's fun, it's music, it's singing, it's laughter," na Nick Minaj
akawa anatikisa kichwa kuonesha anasapoti alichokuwa anasema Mariah Carey.
Wajuzi wa mambo walisema time will tell
sasa kila kitu kinaanza kuonekana hadharani, chanzo kabisa cha kutoelewana kwa
wawili hawa bado hakijajulikana kwa sababu kama Mariah Carey alikata simu pale
tu aliposikia jaji mwenzake atakuwa Nick Minaj, basi chanzo sio kutoelewana
katika maamuzi ya ujaji wao, there must be a long term factor.
Post a Comment