Inaonekana kama
hit make wa don’t wake me up Chris Brown hajakubali kabisa kuwa mbali na ex
girlfriend wake Karrueche hata kama sio kimapenzi tena.
Kwa mujibu wa
Hip Hollywood Chris alimpa ajira kuwa stylist wake, na Karruache Tran aliipokea
ajira hiyo na kumdizainia mtindo wa nywele kwa ajili ya kufanya photo shoot
inayoonekana ni the latest kwa Chris. Ajira hii inasemekana kuwa haina
mahusiano na maisha yao ya kimapenzi bali ni kama wameamua kufanya biashara tu
kwa kuwa Chris anahitaji designer na K.T ni mkali upande huo.
Watu wa karibu
wa wawili hao wameendelea kukanusha kwa msisitizo kuwa hakuna kinachoendelea
kati yao na kwamba Chris Breezy bado yuko na Rihanna wake na anavyokuwa karibu
na K.T haimaanishi kuwa wanataka kurudisha mahusiano yao.
Kwa kawaida
inaleta maswali kwa wengi hasa ukizingatia Chris alitamka hadharani tena
kupitia video aliyoirekodi kuwa anampenda pia Karrueche japo inabidi tu amuache
ili aende kwa Rihanna, na hivi karibuni walionekana anatoka kwake akiwa na K.T
na kumsindikiza na ikasemekana mrembo huyo alienda kuchukua vitu vyake kwa
Chris asepe kwa amani. Ila hii sasa ya kumpa ajira ya kuwa stylist wake katisha
zaidi.
Post a Comment