Imekuwa kawaida sana siku hizi kusikia watu wakizungumza
kuhusu msanii flani ambae amefanikiwa sana, na stori huwa ni kwamba alienda kwa
babu au ni freemason au kamtoa kafara ndugu yake ama hata wazazi wake ili apate
umaarufu huo na pesa. Hali hiyo imewakumba wasanii mapacha waliofanikiwa sana
kimuziki P’Square ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakisema wasanii hao walimtoa kafara mama yao
‘eti’ ili wazidi kuwa maarufu na wapate pesa zaidi.
P’Square ambao wanazidi kupata mafanikio kila dakika na
kuuteka ulimwengu taratibu, walijibu kwa hasira tuhuma hizo, hivi ndivyo
walivyoandika;
“Tunajisikia vibaya sana kujua kuwa mama yetu hayupo tena.
Lakini sisi ni akina nani hadi tumuulize Mungu muweza wa yote. Kwa desturi,
tulitakiwa tumzike na sio vinginevyo. Ila tu imetokea mapema sana. Kiukweli,
kifo chake kilikuwa pigo kubwa kwetu.
“Then, ni mbaya sana kusikia kwamba watu wanatutuhumu sisi
kwa kuwa chanzo cha kifo cha mama yetu. Hatumlaumu mtu yeyote. Watu wako huru
kusema kile wanachotaka kusema. Tumeanza kushangaa endapo kuna kitu ambacho
kingeweza kutusababisha tutumie maisha ya mama yetu.
Maisha yake hayawezi kupimwa kwa kiwango cha pesa wala
umaarufu. Kwa hiyo jibu letu kwa swali hilo ni kwamba hatuna mkono wowote
katika kifo cha mama yetu. Tunakilaumu kifo tu kwa kumnyakuwa mama yetu, na
kama isingekuwa hivyo watu wasingetunyooshea vidole sisi. Alikufa baada ya
kuugua ugojwa kwa muda mfupi sana.”
Haya ndiyo maelezo waliyoyatoa mapacha hawa kutoka Nigeria
wanaotamba na ‘Beautiful Onyinye’ na ngoma kibao kiasi cha kunyakuwa tuzo kibao
na kuongeza umaarufu na mpunga.
- Tujiulize hivi mtu akipata umaarufu na mkwanja inakuwaje akipata tatizo basi inasemekana alitoa kafara, hata akifa yeye mwenyewe utasikia “ooh…freemason wamekasirika wamemchukua”. Duh, we need to think big though dunia ina mambo mengi na hayo yanaweza kuwa ni kati ya hayo mengi na huenda yanatokea kweli kwa baadhi ya watu.
Post a Comment