Roma amekuwa kati ya wasanii wanaotumia sana mitandao ya kijamii vizuri kwa kueleza yake ya moyoni pale anapokuwa na kitu cha kusema.
Kupitia akaunti yake ya facebook, Roma alikuwa na haya ya kusema kuhusu kile kilichotokea na kumfanya aperform chini ya kiwango chake huko Dodoma siku ya Ijumaa iliyopita.
"PAZIA LINAFICHA MENGI SANA!! WATU WASIOFAHAMU MUZIKI NDO WANAPEWA VITENGO MUHIMU KATIKA HII SANAA YETU...
FINALLY THEY
DESTROY THE WHOLE SYSTEM!! INAUMAJE YAANI..
.LAITI UKWELI
UNGEPEWA NAFASI BASI WATU WENGI SANA WANGEAIBIKA DUNIANI HUMU!!! POLE DJ CHOKA
KWA KILICHOKUKUTA DODOMA JANA KWENYE SHOW YA INTERCOLLEGE ROYAL VILLAGE PALE!!
SAMAHANI PIA
WANA DODOMA KWA MIMI KUPERFORM CHINI YA KIWANGO (NILILIONA HILO). NYUMA YA
PAZIA KUNA MENGI SANA MSIYOYAJUA (BACK STAGE).
DAKIKA CHACHE
WAKATI MR BLU ANAMALIZIA KUPERFORM THEN NIENDE MIMI KUMALIZA SHOW. HUKU NYUMA
YA JUKWAA KULITOKEA ZENGWE, KWAMBA DJ CHOKA AMBAYE SIKU ZOTE AMEKUWA NDIYE DJ
WANGU COZ A KNW WAT HE GAT!! WALIMKATALIA ASIPANDE NA MIMI NA BADALA YAKE
NIPANDE MWENYEWE NA DJ WAO, KWA SABABU AMBAZO HAWAKUZITOA(PENGINE NI SABABU
BINAFSI) NA MKATABA HAUKUSEMA HIVO!!
SIKUKUBALI HILI
NA NDIPO HAPO WALIPO NIVURUGA AKILI, TENA WAKASEMA KAMA HUTAKI ACHA KUFANYA
SHOW, KIUKWELI NILIACHA NA KUANZA KUSEPA NA KUELEKEA HOTEL(KAMA NI MBWAI MBWAI
watanga twasemaga)
KWA BUSARA ZA
GODZILLA AKASHAURI NISISEPE NIKUBALI KUFANYA!! MIMI SIKUKUBALI KUFANYA BILA
CHOKA!! SAWA NAWEZA FANYA SHOW NA DJ YEYOTE NA HUWA NAFANYAGA HIVO... BUT KWA
HILI NILISHAWAMBIA NAJA NA CHOKA NA WAKAKUBALI NA KUMUWEKA KWENYE BAJETI YAO!!
KWANINI WAKATAE
MWISHONI!!!??
HATA D.N.A
WALIMFANYIA HIVO NASIKIA NA WAKAMWAMBIA APANDE BILA DJ WAKE. NA YEYE
ALIKUBALI!! (HALIKUNIPENDEZA HILI KWAKWELI)
THANX GOD
NILIKAZA HADI WAKASANDA NA NIKAPANDA NA CHOKA(NDIYO MAANA TULICHELEWA KUPANDA
HADI WENGINE MKAANZA KUSEPA SOORRY DODOMA).
LAKINI SIKUWA
KWENYE MOOD POA KAMA NILIYOKUJA NAYO WALIKUWA WAMESHANIKATA, SO NIKAPERFORM
KIBWEGE SANA.
.LAKINI
NILIFANYA BUSARA KULIKO NINGESEMA NISIFANYE KABISA...MAANA HAMJUI YANAYOTOKEA
NYUMA YA PAZIA!!!
TUNAKUMBANA NA
MITIHANI MINGI SANA LAKINI TUNAIPIGA VITA...ILI TUMAINTAIN NAFASI TULIYOPO.
SIJUI KWANINI
NAPATA VIKWAZO KTK SHOW ZANGU ZA ROUND HII!!
MUNGU TUONGEZE
IMANI NA NGUVU NA HEKIMA NA BUSARA KATIKA KAZI ZA MIKONO YETU!!!
MTWARA KESHO
NIPO NA NYINYI HAPO..TUONE ITAKUWAJE!!
ROMA 2030".
Post a Comment