Diamond Platnumz apata management mpya, shows, mavazi, matangazo, vyote vitasimamiwa na I-VIEW MEDIA.

Mkurugenzi wa I-View Media Raqey na Diamond wakisaini mkataba
Huu ni ukurasa mpya uliofunguliwa na msanii anaefanya vizuri sana hapa nyumbani na nje ya mipaka ya Tanzania Nasib Abdul a.k.a Diamond Platnumz, baada ya kufikia uamuzi wa busara na wa kisomi wa kukabidhi madaraka ya kusimamia na kuendesha shughuli zake za muziki kwa kampuni inayoitwa I-VIEW MEDIA ya jijini Da es salaam.


Baada ya zoezi la kusign contract ya miaka miwili, sasa kampuni ya I-View Media ndio itashughulika moja kwa moja na upokeaji wa bookings na kunegotiate deals zote za msanii Diamond za ndani na nje. 

Hii ni hatua nzuri sana kwa Diamond, sababu hakuna biashara inayofanikiwa bila kuwa na miongozo mizuri ambayo inasimamiwa na watu professionals wa field husika.

Hongera sana Diamond kwa hatua hii muhimu katika career yako.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates