Baada ya kuonyesha uwezo wake kupitia wimbo wake wa kwanza wa "Kifungo Huru" alioutoa mwaka jana 2011, uliofuatiwa na wimbo wake wa pili alioutoa January mwaka huu 2012 unaoitwa "Nishike Mkono", hii ndio single yake ya tatu ambayo kwa mara ya kwanza chiwileinc inakupa nafasi ya kuiona video yake mpya aliyoipa jina la "PAIN KILLER". Wimbo huu umeandikwa na kua produced na Kid bwoy wa Tetemesha Recordz. Video imesimamiwa na Adam Juma wa Visual Lab/Next Level. Kwa mujibu wa management
ya C-sir video itaanza kuonekana katika vituo vya TV mapema wiki Ijayo,
na itaanza kusikika katika vituo vya radio wiki moja baada ya kuanza
kuruka katika Tv stations.
Post a Comment