Rapper mkongwe Nasir bin Olu Dara Jones a.k.a Nas alishindwa
kuhudhuria jana kwenye show yake ambayo ilikuwa inarushwa live kwenye kituo
kimoja cha television kinachorusha show maarufu "Live with Kelly and
Michael!"
Nas kupitia account yake ya tweeter aliwa-update fans wake
kuhusu hali yake ya afya kuwa ilimbidi akimbie kwenda hospitalini muda huo na
kuwaomba radhi kwa kutoonekana kwenye show.
Tweet yake ya january 11 inasomeka hivi, "Peace y'all.
I'm out of the ER & doin alright. I'm on bed rest for a few. Apologies to
everyone @ Live w/ Kelly & Michael. I'll make it up.."
Japokuwa 'hate me now' hit maker hakusema alikuwa
anasumbuliwa na ugonjwa wa aina gani, baadhi ya blogs za Marekani ziliandika
kuwa alikuwa anasumbuliwa na Flu, na kwa mujibu wa 'The YBF' watu wa karibu wa
Nas walimwambia mtangazaji msaidizi wa television show ya "Live With Kelly
& Michael" kuwa Nas alikuwa na Stomach flu.
Post a Comment