Katika kupambana na wale watu ambao hutumia mitandao vibaya kutukana,
kupotosha umma kwa habari za uongo tofauti na maadili yanavyokwenda,
Msanii wa muziki Banana Zorro kwa pamoja na Mrisho Mpoto wameachia wimbo
mpya unaoitwa FUTA, DELETE, KABISA.
Wimbo huu ni kufuatia kampeni ambayo imeanzishwa na mamlaka ya
mawasiliano Tanzania, TCRA kuhamasisha matumizi mazuri ya mitandao ya
kijamii na mawasiliano.
Mkurugenzi wa TCRA , Prof John Nkoma amesema lengo kampeni hiyo ni
kupunguza matusi katika mitandao ya kijamii na kupotosha jami kwa habari
zisizokuwa na uhakika na za kuchochea vurugu.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment