Juliana Kanyomozi, Diva ambaye anafanya poa sana kimuziki nchini Uganda
ameonyeshwa kuguswa kwake na tukio la hivi karibuni huko Iganga Uganda,
la mamlaka ya maji kusitisha huduma ya maji katika hospitali kwa miaka
miwili sasa.
Kufuatia tukio hili ambalo lilifikia hatua ya kuzua maandamano ya wakazi
wa eneo hilo yaliyoingiliwa na polisi, Juliana naye ameamua kutia sauti
yake kuonyesha madhara ya hatua hii ya kusitisha huduma ya maji
hospitali hususan kwa hospitali hiyo ambayo inahudumia watu wanaofikia
500 kwa siku.
Juliana ameungana na wananchi hawa pamoja na mbunge wao Mheshimiwa Peter
Mugema kutaka mamlaka husika kurudisha huduma ya maji kwa hospitalini
hapo, ili kuokoa maisha ya wengi, na kuangalia namna nyingine
wanavyoweza kumaliza deni la shilingi milioni 30 za Uganda ambazo
inadaiwa.
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment