Rabbit aka Kaka Sungura, rapa ambaye anafanya poa hivi sasa katika
chati za muziki mbalimbali Afrika Mashariki kutoka ngoma yake ya Ligi
Soo, ametajwa kama mfano mzuri wa kuigwa kutokana na jitihada zake
zilizomtoa katika maisha ya chini kabisa na hali duni mpaka kufikia
ngazi hii ya Ligi Soo.
Historia ya msanii huyu inaanzia kwenye maisha duni na uhaba wa
fedha ambao ulisababisha yeye kusoma kwa tabu na kufanya biashara za
hapa na pale kabla ya kuingia katika muziki ambapo alianza kama 'backup
singer' wa rapa Chiwawa.
Historia hii yenye mafunzo mengi ya rapa huyu, ni moja kati ya
udhibitisho tosha kwa kila mtu ambaye anajaribu kutumia uwezo wake
kufanya kile anachokipenda kuwa, wakati wote ukijituma mafanikio lazima
yatakufuata
Post a Comment