Rapa mkali wa Sinza Star Mansu-Li, anayeendeleaa kuuwakilisha muziki wa
Hip Hop ambaye baada ya kutoa traki mpya ya kolabo kali na marapa
Jaymoe pamoja na The Don kupitia wimbo wao 'Leo Ndio Leo', hivi sasa
anadondosha project yake mpya ambayo anatarajia kuachia kichupa kipya
kwa mashabiki wake Afrika Mashariki.
Mansu-Li ameiambia eNewz ya Eatv kuwa hivi sasa anatarajia kutoa kichupa kipya ambacho ni wimbo wa kundi lao la 'Kapito Letaz' uliobatizwa jina 'Bado Tupo' ambao wamemshirikisha rapa mkali Godzilla.
Aidha, Mansu-Li aliyejipanga vyema kukonga nyoyo za mashabiki wa miondoko hiyo ameongezea kuwa matayarisho ya project zake hizo yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi katika klabu maarufu siku ya jumapili ya tarehe 18 mwezi huu Jijini Dar es Salaam.
Post a Comment