Wasanii wa muziki wa kizazi kipya wanaofanya poa Hapa Tanzania, Mwasiti
Almasi pamoja na Shetta ambaye kwa sasa yupo huko Kahama kwaajili kuwapa
wananchi burudani ya Eid, Leo hii katika siku hii ya sikukuu ya Eid el
Fitri kwa waislamu sehemu mbalimbali duniani, wamekuwa na ujumbe na
wosia mzito kwa waamini wa dini hii ambao pia ni wapenzi wa burudani.
Kwa niaba ya wasanii na wadau wengine wakubwa katika tasnia hii ya Burudani, Mwasiti pamoja na Shetta wamewataka Waislamu kote nchini kusherekea sikukuu hii kwa amani na pia kuwakumbuka na kusherekea sherehe hii pamoja na wale walio katika mazingira magumu ndani ya jamii.
Sikukuu hii ni moja kati ya sikukuu kubwa hapa nchini ambapo pia wsanii wengine wengi wanakuwa katika shughuli mbalimbali za matamasha kuwaburudisha watu baada ya mwezi mtukufu wa Ramadhani kuisha
Post a Comment