Agnes Gerald ‘Masogange’ katika pozi.
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini
Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na
baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga
waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama
Methamphetamine.Baada ya kuachiwa huru, Masogange anayesifika kwa kuwa na figa matata, alitupia picha hizo katika mtandao wa Instagram akiwa amevalia sidiria na nguo ya ndani pekee hali iliyowafanya wafuasi wa mtandao huo wamshangae huku wengi wakimlaumu kuwa alichokifanya hakifanani na maadili ya Mtanzania.
Video queen grade one Bongo, Agnes Gerald ‘Masogange’.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.
Post a Comment