Drake Amzungumzia Baba Yake Na Anahusika Vipi Kwenye Muziki Na Album Yake Mpya.



Rapper Drake amesema maisha anayoishi sasa ni ndoto ya baba yake mzazi . Drake amefunguka kuwa Baba yake alikuwa na ndoto ya kuwa msanii mkubwa mwenye pesa nyingi ila ndoto yake haikutimia na kwa mapenzi ya Mungu Drake sasa ndio anaishi ndoto ya baba yake.  

Drake pia ameongezea kuwa kwenye album yake mpya 'Nothing Was The Same' ambayo kwa sasa imeshauza kopi milioni Moja yani ni Platinum Album amemshirikisha baba yake kwenye wimbo moja alioupa jina la 'Heat Of The Moment' 

Baba yake Drake, Dennis Graham alikuwa mpiga vyombo kwenye bendi ya zamani ya Jerry Lee Lewis hivi karibuni aliulizwa kuhusu mchango wake kwenye muziki wa Drake na alitoa jibu kuwa "Huwa nasikiliza album yake kabla haijatoka na kumpa ushauri nikiweza".

   

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates