Pamoja na kuwa kuna wanawake husita kuolewa, lakini jambo hili si kubwa sana kwa wanawake kama ilivyo kwa wanaume.
Kwa kiasi kikubwa katika suala la kutaka kuingia ndani
ya ndoa, wanawake ni wengi ambao hutaka kufunga ndoa kuliko ilivyo kwa
wanaume. Hilo tunaliona wazi tokana na shamra shamra awazo nazo mwanamke
wakati wa maandalizi ya shughuli za Ndoa na Harusi.
Hata
hivyo, kwa wale wanawake wachache ambao husuasua kuolewa hizi ni baadhi
ya sababu zinazopelekea kusuasua huko. (Izingatiwe hii ni kwa wanawake
ambao hawajawahi kuolewa kabisa)
Vigezo vilivyopitiliza viwango (hasa kwa muonekano)
Wanawake wengi hasa wa umri mdogo (lakini unatosha kuolewa) hutumia
muda mwingi katika kuchagua aina ya mwanaume ambaye angependa awe mume
wake.Wanawake hawa hujiamini zaidi na kusimamia sifa zile ambazo huamini
ni muhimu mwanaume wa kumuoa awe nazo.
Vigezo hivyo huwa
hata kwa misingi ya muonekano wa mwanaume huyo – kuna wale ambao hutaka
mwanaume huyo wa kumuoa awe na sifa kama vile, mrefu, aliyejazia kifua,
mtanashati, sauti nzuri n.k.
Inaweza kuwa kama mzaha na
ikaonekana ni kipengele kidogo sana lakini bado kuna wale ambao anaweza
kuwa tayari kuolewa ila hataki sababu tu huyo mwanaume hafananii vile
ambavyo yeye anataka mumewe awe.
Kutaka mwanaume tajiri
Kuna wanawake ambao tayari wameshajiwekea akilini kuwa hatakubali kuolewa na mwanaume yeyote yule ambaye hana pesa nyingi.
Yupo tayari kuolewa ila si kwa mwanaume mwenye uwezo wa kawaida – hata
ikitokea mwanaume ana uwezo kidogo wa kuweza kujitosheleza, yeye bado
huona huyo mwanaume hamfai hadi pale tu atakapo pata yule ambaye anahisi
ataishi maisha ya kifahari.
Hivyo hukazana kusubiri na
kujitahidi kuwinda aina ya mwanaume ambaye atakuwa na uwezo mkubwa, bila
kujalisha kama huyo mwanaume kampita sana umri.
Kutompata Mwanaume Ampendae
Hili ni kama tu vile ilivyo kwa wanaume ambao huamini ndoa haiwezekani
na haifai bali tu hadi pale umpatapo yule ambaye unampenda na unaamini
anakupenda pia.
Wengi katika kundi hili huamini kuwa
mafanikio ya ndoa kigezo kikubwa ni kupendana tu na mengine hufuata
kwenye sababu ya upendo. Kunawanawake vigezo vya mwanamme awe vipi
havina umuhimu kabisa katika kutaka kuamua kuolewa.
Yeye
kikubwa anataka ampate mume ambaye atampenda kwa dhati na huku akiwa na
matumaini kuwa huyo mume atampenda na yeye pia kwa dhati. Huyu mwanamke
anaamini msingi bora wa ndoa ni mapenzi ya dhati kati ya yeye na mmewe
basi! Hana haraka hadi pale atakapompata mwanaume akampenda ndipo
atakapokuwa tayari kuolewa.
Kuchagua mno Wanaume wa Kumuoa (SO SELECTIVE)
Kuna wale wachache ambao akili hubadilika kama kinyonga; wasioridhika
wala kujitambua ni nini wanataka ama mwanaume wa aina ipi wanataka.
Akija wa mwenye uwezo atasema nataka wa kuchuma nae, akija asiye na
uwezo atatoa sababu tu hata kama kumlaumu kuwa inaonyesha hajitumi
kutafuta maendeleo.
Akija wa kabila hii, atasema hapana hao
wana tabia hii mimi siitaki! Yaani kwa ufupi ni mtu asiyeisha kutoa
kasoro za wale ambao wanajitokeza kutaka kumuoa.
Hatimaye
inaweza tokea muda wa kuolewa ukapita na akaishia kupunguza uchunguzaji
lakini ikiwa hata wanaume wa umri wa kufaa kumuoa kutokuwepo tena katika
soko.
Kujiona ni mzuri sana
Kuna wanawake ambao ni
kweli Mwenyezi Mungu kawajaalia uzuri hasa (uzuri wa muonekano), anakuwa
ni mzuri kiasi kwamba wake kwa waume wote wanamkubali kwa uzuri huo na
hata wote kumtamani.
Hata hivyo hapo hapo kuna wale ambao huwa
ni wazuri kawaida – ila kwa mtazamowake hujiona ni mzuri mno hakuna
mfano kama yeye; kitendo ambacho kwa wachache kwenye kundi hili hufanya
kujiona yeye ni yeye na kuwa kwa yeyote kuwa na yeye huyo mtu anatakiwa
atambue kuwa ana bahati sana.
Kitendo hiki hukuza nyodo za
hali ya juu ya mwanamke mwenye mtazamo huu, kiasi kwamba wanapojitokeza
wanaume kutaka kuoa – anaweza onyesha tabia kama maringo, dharau na
kiburi.
Kujiona ana Umri mdogo
Binti yeyote wa miaka 18 na kuendelea anaruhusiwa kuolewa endapo tu karidhia kuolewa.
Wanawake wametofautiana mipangilio yao ya kimaisha, kuna wale akiwa
katika umri wa kuolewa hutamani sana kuolewa na kuna wale ambao hupenda
kuolewa wakiwa wakubwa zaidi.
Katika kundi hili umri kuwa
mdogo hutegemeana, kuna mwingine anakuwa na umri wa miaka 25 na bado
akajiona mdogo na hali kuna mwingine anakuwa na miaka 20 na akajiona ni
mkubwa na anafaa kuolewa.
Hii pia ni kwa wanawake wale ambao huwa na malengo ya kutotaka kuharakisha katika ndoa.
Anapokuwa na umri ambao anaweza kuolewa lakini yeye hayupo tayari kwa muda huo, huwa ni kikwazo kwake kuingia katika ndoa.
Maradhi hasa UKIMWI
Hili kama lilivyo kwa wanaume - Pamoja na kuhamasishwa kwingi na
wataalamu wa maradhi ya HIV/AIDS kuwa mtu hata ukiwa umeathirika unaweza
kuwa na mahusiano na hata kuoa na kuwa na watoto; bado haisaidii sana
kwa vijana wanaojitambua kuwa ni waathirika wakiwa bado ni wadogo,
hawajaoa/olewa ama kuwahi kuwa na mtoto.
Wengi sana hukata
tamaa na huona ni kheri kubaki walivyo kuliko kuingia katika ndoa, hasa
tokana na imani kuwa wanawake wakizaa wakati ni waathirika; afya
hudhoofika zaidi.
Kutaka maisha ya Tamthilia (Ndoa za kuishi kwa furaha milele)
Kutokana na kukua kwa idadi ya tamthilia nyingi ambazo huonyesha maisha
ya kimagharibi zaidi; kumekuwa na dhana kwa baadhi ya wanawake kutaka
hayo maisha ya tamthilia yawe na kwao pia.
Hilo linafanya
vigezo ambavyo mwanamke huyo anatumia kuchagua ama kukubali mwanaume
kumuoa kutotimiza yale ambayo yeye binafsi anatarajia.
Wengi
hushindwa kutambua kuwa hakuna maisha ya furaha milele, na hasa kuwa
maisha ya maigizo yapaswa kuchanganya na zako kuweza kufanya maamuzi ya
kipi kiigwe na kipi kiachwe kama kilivyo.
Kuona taasisi ya Ndoa kama Utumwa
Mtazamo huu kwa wanawake wenye msimamo huu, huchangiwa na baadhi kama haya:
- Usomi: Aina ya usomi ambao hupelekea kwa baadhi kuwa na tafsiri tofauti juu ya ndoa, haki, majukumu na mengine mengi.
- Kushuhudia ndoa mbovu: Hii inaweza kuwa ya wazazi/walezi wake wenyewe
(pengine mama aliteswa sana), na hata ndugu wa karibu kama vile
kushuhudia kila ndoa ya ndugu yake anayoijua mwanamke huishi kwa mateso,
manyanyaso na maisha ya taabu na kuonewa.
- Kuwa na uwezo
sana wa kujitosheleza ambao unaweza kumtimizia na kufanya lolote lile
ambalo anataka katika maisha. Kwake kuwa na mwanaume kama mume kwake
anaona kama ni utumwa.
Kutokuwa kabisa na mshipa wa hisia za kufanya mapenzi
Kuna wanawake wale wachache waliozaliwa hivyo. Hawana hisia yoyote ile
ya kimwili ya kuweza kupata hisia za kuweza kujisikia ama kutamani
kufanya mapenzi.
Wengi wa aina hii ya wanawake huwa ni waoga
sana wa kuwa karibu na mwanaume, na kwa wale ambao wamewahi hata jaribu
baadhi huona kama kitendo cha ndoa ni kero, unyanyasaji na uchafu.
Hivyo wazo la kuwa akiolewa anatarajia kufanya kitendo cha ndoa mara kwa mara kinamvunja kabisa hamu ya kutaka kuolewa.
Home » Love story » HIZI NDIZO SABABU 10 ZA WANAWAKE KUTOKUOLEWA NA KUISHIIA KUSAGANA TU
HIZI NDIZO SABABU 10 ZA WANAWAKE KUTOKUOLEWA NA KUISHIIA KUSAGANA TU
By Unknown • 6:34 AM • Love story • Comments : 0
Subscribe to:
Post Comments
(
Atom
)
Post a Comment