Gwiji
la Taarab asilia enzi zilee Msanii Khamis Juma akiwa miongoni mwa
wabunifu na wasanii maalum wanne mwaka huu akikonga nyoyo za washiriki
wa hafla ya zilizofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini
Zanzibar.
Mwenyekiti
wa Kamati ya ugawaji Mirabaha ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la
Rahaleo Mh. Salim Nassor Ali –Jazeera akimkabidhi ngao mchangiaji bora
wa kusaidia sherehe hizo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa
Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Mh.
Salim Nassor – Jazeera akimkabidhi ngao msaidizi wa Makamu wa Pili wa
Rais wa Zanzibar Ustaadhi Suleiman Haji Suleiman akipokea kwa niaba ya
Mhe. Balozi Seif ambae Ofisi yake imegharamia sherehe hizo.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati akimkabidhi
ngao Msanii Khamis Juma baada ya kufuzu kuwa miongoni mwa wabunifu na
wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.
Al
- Anisa Mwapombe Hiari tetere wa nyimbo za Taarabu aliyevuma ndani ya
mwambao wa Afrika katika miaka ile akifurahia zawadi ya ngao na fedha
taslim alizokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif
baada ya kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika
sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.
Msanii
wa Kizazi kipya Baby Jay akipokea zawadi kutoka kwa Balozi Seif kwenye
sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Berry
Black kufurahia zawadi
aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye
sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Balozi
Seif akiwa katika picha ya pamoja na Viongozi wa Kamati ya ugawaji
Mirabaha pamoja na washindi mbali mbali wa tuzo za wabunifu na wasanii
bora kwa mwaka huu mara baada ya kukamilika jkwa sherehe hizo hapo
Ukumbi wa Salama Hoteli ya Bwawani Mjini Zanzibar.
Kushoto
ya Balozi Seif ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mh. Aboubakar
Khamis,Msanii Khamis Juma, Msanii Mwapombe Hiari na Naibu Waziri wa Afya
Zanzibar Mh. Mahmoud Thabit Kombo.
Kulia
ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Mh.
Said Ali M,barouk, Mkuu wa Mkoa wa Mjini Magharibi Mh. Abdullah Mwinyi,
Mjumbe wa Kamati ya Ugawaji Mirabaha Mh. WEanu Hafidh Ameir pamoja na
Mchangiaji bora wa mashindano hayo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje ya
Ushirikiano wa Kimataifa wa Tanzania Mh. Mahadh Juma Maalim.
Post a Comment