Drake Kujenga Studio Kwenye Shule Yenye Wanafunzi Hatari Zaidi Marekani

Rapper Drake wa Young money amesema amehamasika kuishaidia shule ya hatari sana nchini marekani baada ya kuona taarifa ya shule na mazingira yake kwenye vyombo vya habari.


Drake ametangaza kujenga studio ya kurekodi muziki kwenye shule hio ya sekondari inayoitwa Strawberry Mansion iliyopo Philadelphia, Pennsylvania. Shule inawanafunzi 400 na imetajwa kama shule ya hatari sana Nchini Marekani kwa mujibu wa ABC News.

"Nataka kuwajengea studio ya muziki sababu nawapenda, hii ni nafasi yenu ya kufanya kitu na maisha yenu, muwe na maisha mazuri baadae. Kama mtaitumia nafasi vizuri nitafurahi pia" Alisema Drake kwenye mahojiano.

Kwenye interview ya wanafunzi hao, Walisikika wakisema , Hatuna mategemeo na hatuna cha kufanya shuleni na mitaani, Tutaishia pabaya kama kaka na dada zetu.

Tunahitaji kitu kama hichi Tanzania, Haswa kwenye mikoa yenye vipaji visivyo pewa nafasi ya kuonekana. Talent nyingi sana Tanzania ila hazina sehemu ya kuonekana.

Video ya Shule hii na jinsi wanavyo sachiwa iko hapa.

video platformvideo managementvideo solutionsvideo player

Share this:

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates