HIVI NDIVYO MARTIN KADINDA ANAVYOWEZA KUTUNZA SIRI ZA WAREMBO KIBAO WA HAPA BONGO,KAMA WEMA,JACK CLIFF NA WENGINE


MSANII nyota wa filamu Bongo Wema Isack Sepetu amefunguka kwa kudai kuwa hawezi kuvunja urafiki na meneja wake Martin Kadinda kwa sababu kama kuna kitu chochote cha mafanikio nyuma yake yupo Kadinda.

Wema Sepetu ameuambia mtandao wa FilamCentral  kuwa hana rafiki anayejua siri zake zaidi ya meneja huyo ambaye amekuwa akimuongoza vema. 

“Kadinda ndo kila kitu kwangu, hata akiondoka na kukaa mbali na mimi kwa muda mrefu ninapokutana naye tu, nitamweleza kila kitu toka siku ya mwisho tuliyoachana, hivyo inakuwa kama sijapoteana naye,yaani ni kama vile nipo naye kila siku iendayo kwa Mungu,”anasema Wema.

Msanii huyu ameendelea kusema kwamba hata kampuni yake ya Endless Fame film aliifungua kwa msaada wa Kadinda baada ya kumshauri  kuwa kwa hadhi yake anastahili kuwa na kampuni na aache kuigiza filamu za watu wengine.

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates