STORY - TAFAKARI



                                                    
                                                 KUNA WIZI ULITOKEA BENKI
 Jambazi  "wote laleni chini pesa ni za serikali na maisha ni ya kwenu", wote wakalala chini

HII INAITWA DHANA YAUSHAWISHI - kubadilisha njia ya kawaida ya kufikiria

•••••••••••••••••••••• Kuna dada kwa woga akawaamelala chini kimitego,Jambazi akamwambia,


"dada hebu kuwa na adabu chukua kanga jifunike hili ni tukio laujambazi na sio la ubakaji.”

HUU UNAITWA WELEDI -zingatia ulichofundishwa kufanya

••••••••••••••••••••••• Walipotoka kwenye wizi jambazi mdogo ambaye anashahada ya uzamili ya biashara akamwambia mwenzake,

"tuzihesabu hizi fedha.” Yule mkubwa akamcheka kwa dharau na kumjibu, "wewe mjinga sana hizo hazina haja ya kuhesabu saa mbili watatutangazia kwenye taarifa ya habari tumeiba kiasi gani.

HUU INAITWA UJUZI - Siku hizi ujuzi ndio bora kuliko vyeti

••••••••••••••••••••••• Baada ya majambazi kuondoka menejaa kamwambia mhasibu wa bank, " ujumlishie na zile milioni 80 tulizo iba sisi.”

HUKU KUNAITWA KUOGELEA NA MKONDO WA MAJI -kushabihiana na mazingira magumu kwa faida binafsi.

••••••••••••••••••••••• Mhasibu akafurahi na kusema,

"dah wizi ukitokea kila mwezi itakuwa burudani sana.”

HUKU KUNAITWA KUWA NA MAWAZO CHANYA - Furaha ndio kitu cha muhimu zaidi

••••••••••••••••••••••• Meneja kafurahi sana kwakuwa sasa matatizo yake yametatuliwa na wizi uliojitokeza.

HUKU KUNAITWA KUTHUBUTU-shikilia nafasi pale inapojitokeza hata kama nihatari kiasi gani.

••••••••••••••••••••••• Haya usiku wake taarifa ya habari ikatangaza kuwa wizi mkubwa sana wa million 100 umetokea leo benki.

Majambazi kuskia hivyo wakaanza kuhesabu zile pesa lakini wakajikuta na milioni 20 tu. Yule jambazi mkubwa akashtuka na kusema,

"dah!yaani meneja kaiba mara nne zaidi yetu bila kuchezeshamsuli? Bora umeneja kuliko ujambazi.

”HII INAITWA ELIMU NDIYO KILA KITU - ishike sana elimu ina nguvu kuliko dhahabu

Share this:

Post a Comment

 
Copyright © CHIWILEINC. Designed by OddThemes | Distributed By Gooyaabi Templates